WATENDAJI KATA WAKUMBUSHWA KUHIFADHI VIZURI TAARIFA ZA LISHE NA UFUATILIAJI WAKE

Na Jackline Kuwanda, Dodoma.

Watendaji wa kata wametakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa na namna nzuri ya kuhifadhi taarifa za lishe pamoja na ufuatiliaje wake.

Wito huo umetolewa leo na Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma  Innocent Daniel Kess katika Kikao cha Tathimini kuhusu mkataba wa lishe kwa ngazi ya kata ambao umefanyika jijini hapa.

‘’mikataba ya lishe ndani ya ngazi kata ukuwauliza wenzenu wa mikoa mingine tayari wamefanya sasa sisi ambao ndio wa makao makuu ya nchi ndo hatajufanya kama mfefanya basi ni wachache sana ,kwa maelekezo niliyopewa  kwa wale ambao hawajaleta mlete ijumaa ya wiki ijayo kwasababu huyu anaandaa taarifa zinazoenda kwenye ngazi za juu atapataje hizo taarifa ni mpaka ziwe zimekuja’’ Kess

Kwa upande wa Afisa Lishe Mkoa wa Dodoma Heriet Carin amesema jukumu la kukusanya taarifa za lishe ni moja ya kazi zao lakini pia kuwa na jukumu la kuhusika katika kuwaratibu wadau wowote wanaokwenda katika kata zao.

‘’mnatakiwa kuwaratibu wadau wowote wanaokuja katika kata zenu na tunapokuja hapa tunatakiwa tuwe na ulewa wa mambo yote’’

Naye Afisa Lishe wa Jiji la Dodoma Seminieva Juma amesema  Mikataba hiyo ya lishe imekuwa ikitekelezwa katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya Taifa , Mkoa ,Halmashauri ,wilaya ,kata mpaka mtaa.

‘’kwa kuanzia tumeaanza na robo hii ya julai /septemba robo ya kwanza ya mwaka  wa fedha 2020/2021 juu ya tathimini iliyofanyika katika jiji la dodoma kuhusiana na masuala yale ya lishe’’Seminieva

Mwisho.


Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.