Na Faruku
Ngonyani,Mtwara
Wananchi wa kata ya
Naliendele iliyopo Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara
wamelalamikia juu ya ukosefu wa maeneo ya kujenga maeneo ya huduma muhimu za
kijamii kama vile Shule, eneo la makaburi ,Soko pamoja eneo la zahanati.
Hayo wameyazungumza
mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstani Kyobya kwenye Mkutano wa hadhara
uliyofanyika katik eneo hilo ukiwa na lengo kwa Mkuu wa Wilaya la kusikiliza na
kutatu kero za wananchi hao.
Wananchi hao wamesema
kuwa kwa sasa wanakosa maeneo ya huduma ya kijamii kwa kuwa maeneo yaliyo mengi
yamechukiliwa na Taasisi mbalimbali za kiserikali wakiwemo baadhi yao kiwa ni
kituo cha Utafiti cha Kilimo Naliendele,Chuo cha Kilimo,jeshi la wananchi
pamoja na mamlaka ya uwanja wa Ndege.
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Mtwara Dunstani Kyobya ametoa mwezi mmoja kwa wataalam wa ardhi
kutoka Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani kuhakikisha wanaenda kufanya
utafiti ili maeneo hayo yaweze kupatikana na wananchi waweze kujenga nyumba
za kupata huduma muhimu za kijamii na makazi yao.
Aidha Mkuu huyo wa
Wilaya ametoa agizo kwa Chuo cha utafiti cha kilimo Naliendele kutoa elimu kwa
wananchi wa kata hiyo ya Nalinendele ili waweze kufahamu na kujua umuhimu wa
kuwa na chuo hiko katiuka eneo hilo.
Lakini pia Mkuu huyo wa
Wilaya ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Manispaa
Mtwara Mkindani kutoa Notes ya miezi kwa Mtu yeyote asiyeendeleza maeneo yao na
hatmae kunyang’anywa maeneo yao.
“Wale wote ambao
wanamaeneo yao hayajaendelezwa wenye hati na wasikuwa na hati kanini
wasipewe notes ya kunyang’anywa maeneo hayo kwa kutoyaendeleza’’
MWISHO.
Comments
Post a Comment