DODOMA.
SERIKALI imeajiri walimu wapya wa shule za msingi,sekondari pamoja na mafundi sanifu wa maabara elfu 13 huku ikiwataka walimu hao kuripoti katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa ndani ya siku 14 kuanzia disemba mosi mwaka huu.
Miongoni mwa walioajiriwa asilimia 60 ni walimu wa shule za msingi wakiwemo walimu wenye shahada 1,100 na asilimia 40 ni walimu wa shule za sekondari.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Ofisini kwake jijini Dodoma Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema ajira hizo zinatokana na kibali kilichotolewa na Rais Dokta John Magufuli septemba 7 mwaka huu.
Mhandisi Nyamhanga ametoa maelekezo matano kwa waajiriwa hao wapya ikiwemo kuhakikisha wanaripoti katika eneo walilopangiwa kwak uwa hakuna mwajiriwa atakayebadilishiwa kituo kwa kipindi cha miaka mitatu.
Waajiriwa hao wanatakiwa kuripoti wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne na kidato cha sita, vyeti halisi vya kitaaluma vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ya ngazi husika,kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho ya NIDA na cheti halisi cha kuzaliwa.
Mwisho.
Comments
Post a Comment