DODOMA.
WAKULIMA wa Wilaya ya Bahi wameshauriwa
kuchangamkia mvua ambazo zimeanza kunyesha kwa hivi kwa Kanda ya Kati kuandaa
mashamba mapema na kupanda mbegu za kisasa zinazokomaa kwa haraka.
Ushauri huo umetolewa Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania Askofu Julias Bundala alipokuwaa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nhyinila kata ya Mtita wilaya ya Bahi wakati wa ibada ya shukurani iliyofanyika kiijiini hapo.
Bundala alisema kuwa kanda ya kati hivi sasa mvua zimeanza kunyesha, hivyo zichangamkie kwa kuandaa mashamba na kupanda mbengu bora za kisasa zitakazokoma haraka.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho alisema mvua ambazo zimeanza kunyesha ni muhimu zikachangamkiwa uknzingatia kuwa mara nyingi zinakuwa za muda mfupi tofauti na mikoa mingine ambayo imekuwa ikinyesha kwa wingi.
Alisema ili waweze kufikia malengo hayo ya kilimo cha kisasa kwa malengo ya mafanikio ,wanatakiwa pia kuacha na kilimo cha mazoea ambacho hakina tija kwa mkulima.
Askofu huyo pia amewataka kuhakikisha wanawaaomesha watoto wao,ili waweze kufikia ndoto walizonazo badala ya kuwaacha majumbani na wengine kuwafanyisha kazi za ajira za majumbani.
Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa hilo la Pentecostal Holiness Association Mission Sinai Nhinila Peter Chabwalo,amewaomba wanakijiji kuendelea kuombea serikali ili iweze kufikia maendeleo ambayo Rais Dk John Magufuli amekuwa akisisitiza
Aidha amewaomba vijana kufanya kazi kwa malengo ili waweze kufikia ndoto zao,badala ya kujiingiza kwenye makundi ambayo yanayopotosha na kusababisha umaskini.
Mwisho.

Comments
Post a Comment