Wafanyabiashara nchini walia na Wachina

 Na Rhoda Simba, Dodoma. 

JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) wameilalamikia Serikali kitendo Cha wafanyabiashara wa Kichina kuingilia  soko na kuuza bidhaa zinazouzwa na wazawa.

Aidha jumuiya hiyo ilisema Wachina hao wanafanya biashara za kichuuzi ambazo zinafanywa  na wafanyabiashara wadogo wasafi  alimaarufu Kama Wamachinga hivyo kufanya mazingira ya Biashara kwa wazawa kuwa magumu.

Akizungumza Jijini hapa katika mkutano wa wenyeviti na makatibu wa  jumuiya hiyo Mwenyekiti wa JWT  Silva Kyando amesema kuwa Wachina hao wanafanya mazingira ya Biashara kwa Wamachinga hususani wa Kariakoo kuwa magumu

" Unajua Wachina Kule  kwao wanapata mikopo yenye riba nafuu kuliko sisi hivyo wakileta.biashara hapa chini Wana uwezo wa kuuza Bei ya chini kuliko mfanyabiashara mzawa, Sasa hiyo inaua sok la Wabongo", alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema kuwa Wachina Kule kwao wanapewa mikopo yenye yenye riba kuanzia asilimia 6 Hadi asilimia 5.5,wakati mikopo inayotolewa hapa nchini ni asilimia 20 hadi 40.

Aidha.Kyando alisema kuwa Wachina hao wamekuwa wakilindwa na.Mamlaka husika hata wakipeleka malalamiko yao hayasikilizwi hivyo wanajikutaa wanaishi katika nchi yao Kama watoto Yatima.

" Tunawapenda Wachina ni marafiki zetu wa muda mrefu,lakini hatutaki kuingiliwa soko letu ,wao ni wawekezaji siyo kuja kufanya Biashara ambazo Wamachinga.wanafanya", alisema Kyando.

Mbali na hilo Mwenyekiti huyo alisema kuwa kutokana na.mazingira ya kulindwa Wachina.hao wamekuwa wakwepaji Kodi wakubwa kwani Kuna wakati wanashusha makontena hakuna risiti za EFD Wala leseni hivyo wanajikutaa wakiuza kwa faida kubwa.

Mwenyekiti huyo amesema Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John  Magufuli ni sikivu .wanaamini Changamoto ya Wachina itafanyiwa kazi.

Aidha mbali na Changamoto ya Wachina Mwenyekiti huyo amesema tozo ya Service levy ni kero kubwa kwa Wafanyabiashara hivyo wanaomba Serikali ifute kwani wao siyo walengwa.

Kyando pia aliitaka Serikali kutumia hekima  kuwatafutia maeneo maalum ya kufanyia Biashara Wamachinga kuliko kupanga bidhaa za mbele ya maduka.

Unakuta Mmachinga kapanga bidhaa zake mbele ya duka ambalo na lenyewe lina uza bidhaa ileilei hivyo wanawazibia riziki wenye maduka kwani wao wanauza kwa Bei ya chini.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa Dkt. Godwin Wanga alisema Serikali imo pamoja na wafanyabiashara hao, ambapo aliahidi Changamoto hizo zitapelelwa sehemu husika.

Mwisho.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.