TAHADHARI KUHUSU WAGONJWA NA NDUGU ZAO WANAOCHANGISHA FEDHA ZA MATIBABU YA MOYO KWA AJILI YA KUTIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI)
Uongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) unapenda kuutahadharisha Umma kuwa waangalifu na wagonjwa wanaochangisha fedha kwa ajili ya kutibiwa katika Taasisi hii.
Ndugu Mwananchi, inawezekana wagonjwa hao
wanaochangisha fedha za matibabu wanakuwa tayari wamepata msamaha wa
matibabu kutoka kwa Taasisi au wasamaria wema wamewalipia.
Hivi karibuni kumezuka tabia ya baadhi ya wagonjwa au
ndugu zao ambao siyo waaminifu wanachangisha fedha za matibabu kwa wananchi
wakati tayari wameshapata msamaha wa matibabu kutoka kwa Taasisi au kutokuwa na
tatizo ambalo gharama za matibabu yake zinahitaji kiasi kikubwa cha fedha.
Kama utakutana na tangazo la aina hiyo kabla
hujamsaidia mhusika tafadhali wasiliana na uongozi wa Taasisi kupitia namba
0222152392/0782-042010/0688-
Imetolewa na:
Anna Nkinda
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
27/11/2020
Comments
Post a Comment