TAHADHARI KUHUSU WAGONJWA NA NDUGU ZAO WANAOCHANGISHA FEDHA ZA MATIBABU YA MOYO KWA AJILI YA KUTIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI)
Uongozi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) unapenda kuutahadharisha Umma
kuwa waangalifu na wagonjwa wanaochangisha fedha kwa ajili
ya kutibiwa katika Taasisi hii.
Ndugu
Mwananchi, inawezekana wagonjwa hao wanaochangisha fedha za matibabu wanakuwa
tayari wamepata msamaha wa matibabu kutoka kwa Taasisi au wasamaria
wema wamewalipia.
Hivi karibuni
kumezuka tabia ya baadhi ya wagonjwa au ndugu zao ambao siyo waaminifu
wanachangisha fedha za matibabu kwa wananchi wakati tayari wameshapata msamaha
wa matibabu kutoka kwa Taasisi au kutokuwa na tatizo ambalo gharama za matibabu
yake zinahitaji kiasi kikubwa cha fedha.
Kama
utakutana na tangazo la aina hiyo kabla hujamsaidia mhusika tafadhali wasiliana
na uongozi wa Taasisi kupitia namba 0222152392/0782-042010/0688-
Imetolewa na:
Anna Nkinda
Mkuu wa
Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete
27/11/2020
Comments
Post a Comment