RAIS MAGUFULI AWASHUKURU VIONGOZI WA DINI KWA KULIOMBEA TAIFA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO

 

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru viongozi na waumini wa dini ya kiislamu pamoja na wa dini nyingine nchini kwa kuliombea Taifa katika kipindi cha miaka mitano ya awamu ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano na amewasihi waendelee na utaratibu huo.

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa, Novemba 27, 2020 baada ya kuswali swala ya Ijumaa katika msikiti wa Msalato jijini Dodoma. “Wakati najiandaa kuja kuswali nilimuaga Mheshimiwa Rais na ameniagiza nilete salamu zenu kwamba anawashukuru sana kwa kumuunga mkono.”

Waziri Mkuu amesema: “Rais Dkt. Magufuli amesema mbali na viongozi hao na waumini kumuunga mkono katika awamu ya kwanza ya uongozi wake, pia walitoa ushirikiano mkubwa katika kipindi cha kampeni kwa kuendelea kuliombea Taifa hadi uchaguzi ukafanyika kwa amani.”

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.