Na Jackline Kuwanda, Dodoma
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugani amesema ni jambo lisilokubalika kwa mtu yeyote kudharau shughuli za Bunge ,kudhalilisha Bunge,kudhalilisha uongozi wa Bunge na hata kudhalilisha wabunge ambao tayari wamekwisha kuapishwa.
Ndugai ameyasema hayo leo Jijini Dodoma katika Hafla ya uapishaji wabunge wateule katika viwanja vya Bunge jijini hapa.
Aidha Ndugai amesema wabunge wote walioapishwa wanatambulika kama wabunge halali wa Bunge la 12 wakiwamo wabunge 19 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Wakati huo huo Mh Ndugai amewataka watanzania kupiga vita ukandamizaji dhidi wanawake katika jamii zao kwa kisingizio chochote kile huku akimuonya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa kitendo cha kutoa maneno ambayo si mazuri dhidi ya wanawake walioapishwa hivi karibuni akiwemo Halima Mdee pamoja na wenzake.
''ni aibu kubwa kutukana wanawake hadharani napenda kumuonya na kumkanya mwenzangu asione sifa katika jambo hilo wanawake ni mama zatu,dada zetu,shangazi zetu hata kama wamekosea namna gani tuwatafute tukae nao,tupate maelezo yao na sio kuwafukuza kama vibaka'' Ndugai
Hatahivyo, Mh Ndugani ametoa wito kwa waandishi wa Habari kuwa na weledi ya kutosha kuhusu shughuli za Bunge na kutokuwa sehemu ya kisikiliza upotoshaji unandolea.
MWISHO.
Comments
Post a Comment