Na
Rhoda Simba Dodoma.
MRADI
wa Tuimarishe Afya wa (HPSS) unaofadhiliwa na Serikali
ya USWIS chini ya shirika la Maendeleo la SDC Swis Agency For Development
and Copperation umejipanga kuboresha mfumo mzima wa afya nchini kwa
kutekeleza miradi mbali mbali kupitia serikali.
Hayo
yamesemwa jana jijini Dodoma na Meneja Mradi Ally Abdallah wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la saba la
wadau wa afya nchini( Tanzania Health Summit).
Aidha
amesema kuwa lengo la mradi huo ni kutekeleza miradi ambayo
italeta matokeo chanya na kuonekana katika jamii na unafanya
uboreshaji katika mfumo wa afya, mfumo wa fedha, mfumo wa vifaa tiba, na
mfumo wa upatikanaji wa dawa.
“Mfano
wa mifumo hiyo ni pamoja na CHF iliyoboreshwa mfumo wa upatikanaji
wa dawa (Jazia PVS)na Mradi huu upo hapa katika maonesho ili kuchangia tija
katika masuala mazima ya mfumo wa afya nchini, kuchangia mifumo ya afya
nchini, pamoja na kujifunza.”amesema Abdallah.
“Kwa
kuwa kila tunachokifanya lazima kilete matokeo kwahiyo sisi tupo hapa ili
kuonesha miradi tuliyoifanya na si vinginevyo” amesema Abdallah
Amesema
Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS,) ni mradi mkubwa na wenye mafanikio
kwani upo hadi kwenye ilani inayozungumzia upatikanaji wa dawa
nchini.
Hata
hivyo Abdallah amesema wao wamejipanga kuendelea kutoa elimu katika
banda lao kwenye kongamano hilo la saba la wadau wa afya
kwani kupitia wadau hao ndipo wanapopata fursa zaidi ya kuutangaza mradi na
kujitangaza kwa jamii kwa ujumla.
MWISHO.

Comments
Post a Comment