Mfumo wa eHMS wasaidia kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito na watoto nchini

Na Rhoda Simba, Dodoma

MFUMO wa eHMS unaofanya kazi katika idara ya afya umesaidia kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito  na watoto wachanga nchini.

Hayo yameelezwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi mtendaji wa GPITG LIMITED Adelard Kiliba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la 7 la wadau  wa afya nchini Tanzania Health Summit.

Mfumo huo umewezwa kusambazwa katika taasisi 40 ikiwemo hosptali ya Bugando KCMC na taasisi zingine huku kazi kubwa ni kufanya muungano hasa kwa upande wa bima ya afya kwa kuondoa makaratasi na kutumia mfumo wa kielektroniki inayowasaidia madaktari "alisema.

 

MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.