KUNDI LA VIJANA HATARINI KUPATA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI

 




Na Jackline Kuwanda, Dodoma.

Tathmini ya hali ukimwi hapa nchini inaonesha kuwa kundi la vijana kuanzia miaka 14-25 ni miongoni mwa makundi ambayo yako hatarini kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi .

Hiyo ni katika kuelea kwenye maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani inayoadhimishwa tarehe 1 Disemba ya kila mwaka ambayo kwa mwaka huu yanakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘’Mshikamano wa Kimataifa,Tuwajibike kwa pamoja’’

Akizungumza leo katika kongamano la vijana lilofanyika jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square Tumsifu Mwasamale ambaye ni Afisa Maendeleo ya vijana mwandamizi Mkoa wa Dodoma amesema linapozungumziwa suala la ukimwi katika nchi kundi hilo la vijana ndilo linaloongoza.

‘’kwa tafsiri yake ni kwamba kama nchi kama wadau bado tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye kundi hili kubwa la vijana, sababu ziko nyingi changamoto ni nyingi ,ni kundi linalokuwa damu inachemka wakati mwingine si rahisi sana kujizuia kuingia kwenye matamanio yanayowapelekea kuingia kwenye maambukizi ya virusi vya ukimwi ndiyo sababu kubwa’’ Mwasamale

Eriko kawanga mratibu wa masuala ya ukimwi ngazi ya Mkoa amesema lengo la kongamano hilo ni kutaka watu kupata elimu zaidi kuhusu masuala ya ukimwi.

‘’katika masuala ya maambukizi ya ukimwi bado maambukizi mapya yapo kuna watu wamejisahau kuchukua hatua mapema kujua hali zao nawapongeza wale ambao wanachukua hatua za kwenda kupima ili kujua hali zao lakini nawapongeza wale pia ambao wanaishi na virusi vya ukimwi sababu tayari wameshajua hali zao’’Kawanga  

Akisoma taarifa fupi ya Taasisi ya Education and Social Aid Pioneers (ESAP) inayojishughulisha na utoaji Huduma Elimu na Misaada kwa jamii Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Joel Said Katala amesema wamefanikiwa kuandaa kongamano la vijana lililowapa fursa ya kutoa elimu mbalimbali kwaajili ya makuzi na malezi ili kuwaelimisha vijana jinsi ya kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kupelea kupata maambukizina virusi vya ukimwi.

Nao vijana walioshiriki katika kongamano hilo akiwemo Lucy Simon amesema kupita kongamano hilo wamepewa maelekezo na elimu ya namna ya kujikinga na ugonjwa huo na wao kama vijana watazingatia huku Sabri Nassor akisema elimu hiyo kwa vijana ni muhimu kuzingatia kwani itawasaidia wao kujiepusha kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.

MWISHO.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.