KITUO CHA MBEZI LUIS CHAANZA RASMI MAJARIBIO

 

Kituo kipya Cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi Cha Mbezi Luis kimeanza rasmi majaribio jana ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amesema kwa Sasa kituo hicho kinaweza kuanza kutumika Kutokana na miundombinu muhimu ya kituo kuwa Katika Hali mzuri.

 

Akizungumza wakati wa zoezi la majaribio lililowahusisha Askari wa usalama barabarani na Wadau wa vyombo vya usafiri, RC Kunenge ameshuhudia Mabasi yakiingia na kutoka pasipo usumbufu wowote.

 

Aidha RC Kunenge amesema kwa Sasa kinachoendelea ni matengenezo madogomadogo ya umaliziaji wa jengo na miundombinu mingine ambapo Hadi Sasa Ujenzi umefikia zaidi ya 90%.

 

Pamoja na hayo RC Kunenge amesema Ujenzi wa barabara ya kuingia kituoni hapo nao unaendelea vizuri chini ya Wakala wa TANROAD ambapo amewahimiza kuongeza kasi ili wakamilishe mradi mapema.

 

Hata hivyo RC Kunenge ameongeza kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha maagizo ya Rais Dkt. John Magufuli ya kutaka Ujenzi ukamilike mwishoni mwa mwezi huu yanatimia.

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.