Na Rhoda Simba, Dodoma.
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Prof. Mabula Mchembe amezitaka Hospitali za Rufaa zote nchini kuwa na ubunifu mahususi wa kutengeneza vitu mbalimbali kama kipindi cha Corona jambo ambalo litasaidia Taifa kutokupoteza Fedha kwenda nje ya nchi.
Ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati alipokuwa kwenye Maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa Kwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa dodoma (General) .
Aidha Katibu huyo amesema kuwa kuna haja ya Hospitali zote kuwa na ubunifu mbalimbali wa kutengeneza vifaa ambavyo nchi imekuwa ikitumia pesa nyingi kwenda nje ya nchi kuvinunua jambo ambalo sio sahihi kwani wapo wataalamu wenye vipaji na ujuzi mkubwa.
"Niwasihi msibweteke amka anzeni kutumia vipaji vyenu kulisaidia Taifa letu nakumbuka wakati wa kupindi cha Ugonjwa wa Korona mlijitahidi kutengeneza vifaa mbalimbali ikiwemo barakoa,vitakasa mikono na makoti hali iliyosaidia kwa kiasi kikubwa kutoa huduma kiurahisi"
"Nashauri ni vyema kila Hospitali kuwepo na kitengo hicho na kikatengeneza maji ya Drip kwani wagonjwa wengi wamekuwa wakihangaika pale wanapokuta yameisha kwa kufanya hivyo itatusaidia Serikali na Hospitali kuwa na maendeleo makubwa "amesema Katibu mkuu Profesa Mchembe.
Katika hatua nyingine aliwataka wafanyakazi kuwa na kasumba ya kufanya kazi kwa upendo ,kusaidiana ,kuelekezana, kufundishana,kujifunza na kushirikiana kwa watu wote bila kujali vyeo walivyo navyo na kwa kufanya hivyo huduma itafika mbali .
"Na katika kufanikisha shughuli za ujenzi niwashauri muwe mnawatumia watu wa magereza ambao watafanya kwa haraka na gharama nafuu na pesa zinazobaki zitasaidia kufanya kununua madawa"alisema
Nae Mganga mfawidhi wa Hospitali ya General Daktari Ernest Ibenzi alisema tangu kuanzishwa kwa hispitali hiyo kupitia Serikali na waasisi mbalimbali waliopitia ambao walifanya kazi kubwa ya kuboresha miundo mbinu.
Kuwa mbali na mafanikio makubwa yaliyopo katika utoaji huduma za afya bado kuna changamoto licha ya Serikali ikuendelea kuzitatua .
"Bado tuna upungufu wa watumishi, Majengo mbalimbali na ukosefu wa uzio imara,vifaa na majengo ya mifupa tunaomba Serikali iweze kutusaidia ili tuweze kufanya kazi kwa viwango stahiki"alisema Daktari Ibenzi.
Bertha Bahati ni mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo alisema kuwa huduma inayotolewa inaridhisha kwani wanapata madawa kwa wakati,wanasikilizwa vizuri tofauti na kipindi cha nyuma .
"Tunamshukuru sana
Rais wetu John Magufuli amerudisha heshima kwenye Hospitali nyingi siku hizi
unapofika hospitali tunapewa huduma zote na kwa haraka na hakuna tena ubaguzi
kama zamani ambapo ungekaa kwenye foleni asubuhi mpaka jioni bila kusikilizwa
na kunyanyapiliwa"alisema Bertha.
MWISHO
Comments
Post a Comment