JUMLA YA WAHITIMU 5753 CHUO CHA HOMBOLO WAASWA KWENDA KUTUMIA UTAALAMU WALIOUPATA CHUONI

 


DODOMA.

Jumla ya wahitimu 5,753 waliohitimu mafunzo katika fani mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2019/2020  katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma wametakiwa kwenda kufanya kazi kwa weledi wakitumia utaalamu walioupata chuoni hapo.

Wito huo umetolewa na katibu mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga wakati akitoa hotuba katika mahafali ya 12 ya chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo yaliyofanyika chuoni hapo.

Nyamhanga amesema kuwa chuo kinapaswa kuendelea kutoa elimu bora na kwamba wahitimu nao wanatakiwa kwenda kufanya kazi katika mazingira yeyote na kuacha kuchagua sehemu za kufanyika kazi kwa kuyakwepa maeneo ya Vijijini kutokana na visingizio mbalimbali.

Aidha amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa wahitimu wa chuo hicho wakati wa kutoa ajira kwani wahitimu hao ni wabobezi kwenye taaluma ya serikali za mitaa na hivyo kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuleta ufanisi zaidi.

Awali Mkuu wa chuo hicho Dkt.Mpamila Madale amesema chuo kinatarajia kuanza ujenzi wa madarasa mengine, kukarabati kumbi za mikutano na bwalo la chakula, kama moja ya mipango katika kuboresha elimu chuoni, ambapo pia ameiomba Serikali kusadia kuongeza mabweni na kufanya ukarabati wa barabara ya Ihumwa hadi Hombolo ili kuondoa changamoto ya ajali zinazosababishwa na ubovu wa barabara hiyo.

Baadhi ya wahitimu katika chuo hicho wamesema wamejipanga kwenda kukabiliana na tatizo la ajira kwa kujiajiri wenyewe katika sekta mbalimbali ikiwamo biashara na kilimo na kwamba watatumia utaalamu walioupata katika kukamilisha malengo na ndoto zao.

Mwisho.


Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.