Na
Rhoda Simba Dodoma.
MRADI
wa Tuimarishe afya wa (HPSS) unaofadhiliwa na Serikali ya Uswis
chini ya shirika la Maendeleo la SDC Swis Agency For Development and
Copperation umejipanga kuboresha mfumo mzima wa afya nchini kwa
kutekeleza miradi mbali mbali kupitia serikali.
Ally Abdallah |
Hayo
yamesemwa leo jijini Dodoma na Meneja mradi Ally Abdallah wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la saba la wadau
wa afya nchini (Tanzania Health Summit).
Aidha, amesema kuwa lengo la mradi huo
ni kutekeleza miradi ambayo italeta matokeo chanya na kuonekana
katika jamii na unafanya uboreshaji katika mfumo wa afya, mfumo wa
fedha, mfumo wa vifaa tiba, na mfumo wa upatikanaji wa dawa.
“Mfano
wa mifumo hiyo ni pamoja na CHF iliyoboreshwa mfumo wa upatikanaji wa
dawa (Jazia PVS)na Mradi huu upo hapa katika maonesho ili kuchangia tija katika
masuala mazima ya mfumo wa afya nchini, kuchangia mifumo ya afya nchini,
pamoja na kujifunza.” amesema Abdallah.
“Kwa
kuwa kila tunachokifanya lazima kilete matokeo kwahiyo sisi tupo hapa ili
kuonesha miradi tuliyoifanya na si vinginevyo” amesema Abdallah.
Amesema
Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS,) ni mradi mkubwa na wenye mafanikio
kwani upo hadi kwenye ilani inayozungumzia upatikanaji wa dawa
nchini.
Hata
hivyo Abdallah amesema wao wamejipanga kuendelea kutoa elimu katika
banda lao kwenye kongamano hilo la saba la wadau wa afya
kwani kupitia wadau hao ndipo wanapopata fursa zaidi ya kuutangaza mradi na
kujitangaza kwa jamii kwa ujumla.
Aidha, amesema mfumo huo unamsaidia mgonjwa kuhudumiwa kwakutumia na madai ya mgonjwa huyo anayotakiwa kulipwa yanatumiwa bima ya Afya.
Pia amesema mfumo umeunganishwa na mashine za maabara na mashine ya mionzi ambayo inasaidia kuondoa na kupunguza kabisa ubadhilifu wa fedha kwani mfumo huo unatoa taarifa moja kwa moja karika hositali husika kwa kila hatua huduma aliopata mgonjwa.
Amesema kuwa mfumo huo ni mfumo wa kitanzania uliotengenezwa na watanzania ambao umesaidia kurahisisha kazi katika sekta ya afya nchini.
Aliongeza kuwa mbali hayo aliongeza katika kukuza uchumi wa kati lengo ni kuleta afya bora ambapo ni muhimu kuboresha miundo mbinu jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya vifo vya mama na mtoto kwani mfumo huo umeunganishwa na maabara kuangalia maendeleo yake.
Katika hatua nyingine alisema mfumo huo kazi zake ni kurahisisha huduma ya afya kuanzia mapokezi hadi huduma nzima ayakayo pata mgonjwa hospitalini.
Aidha, aliongeza kuwa wameweza kupata mafanikio makubwa katika utaratibu wa afya huku wakiongeza ufanisi kwenye utendaji kazi ambapo pia kufanya kazi kwa njia ya mfumo wa kielektroniki inayowasaidia madaktari .
MWISHO
Comments
Post a Comment