DODOMA.
Tafiti zinaonyesha kuwa robo tatu ya watoto walio na umri kati ya miaka 2 hadi 4 duniani kotesawa na watoto milioni 300 wanakumbana na ukatili unaodhaniwa ni kuwafunza nidhamu kutoka kwa wazazi au watu wanaowalea wakiwa nyumbani.
Ripoti hiyo ni kulingana na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto UNICEF ilioyotolewa mwaka jana ambapo inaeleza kuwa zaidi ya watoto milioni 250 wanakumbana na adhabu ya kupigwa pamoja na mateso mengine wanayofanyiwa majumbani pamoja na maeneo mengine wanayokusanyika kujifunza ikiwemo mashuleni.
Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya wazazi jijini Dodoma ili kufahamu ni kwa namna gani wanaweza kuwafunza nidhamu nzuri watoto wao bila kuwafanyia ukatili ambapo wamesema kuwa wazazi wengi wanaamini kuwa kumchapa au kumpiga mtoto ndio kumfunza nidhamu jambo ambalo si sahihi kwani mtoto anaweza akafundishwa adabu nzuri pasipo kupigwa bali kwa kumuwekea misingi mizuri ya kutambua jambo jema na baya.
Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi wa dawati la jinsia na watoto wa jeshi la polisi Mkoani Dodoma Thelesia Mdendemi amewataka wazazi kujenga mazoea ya kumzungumza na watoto wao mara kwa mara kwa kuwa hiyo itasaidia kuwajengea nidhamu nzuri bila kuwapiga au kuwapa adhabu .
Amesema kuwa wazazi wengi wanaamini kuwapa adhabu au kuwapiga watoto wao
ndio kuwafundisha adabu nzuri jambo ambalo sio sahihi kutokana na hali hiyo
kumuathiri zaidi mtoto kifikra na kimwili.
Suala la ukatili wa dhidi ya watoto linatokea kila mahali kwa sura tofauti
tofauti kulingana na mazingira anayoishi mtoto ambapo ripoti ya shirika la
watoto Duniani inathibitisha dhana hiyo na kueleza kuwa watoto wanakutana
na ukatili katika hatua zote za ukuaji wao katika mazingira wanayoishi.
Mwisho.
Comments
Post a Comment