Kongwa, Dodoma.
WAKULIMA wa kijiji cha Leganga wilayani Kongwa
wamemuomba Rais
kuingilia kati mgogoro uliopo wa muda mrefu kati yao na jamii ya wafugaji wa
kimasai ambao wanaodaiwa kukata miche ya mikorosho iliyooteshwa ikiwemo na
kulisha mifugo kwenye mashamba yao.
Ombi hilo limetolewa na mkulima Mashaka Chiloa kwa
niaba ya wakulima hao walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari.
Chiloa alisema kuwa wanalazimika kumuomba Rais ili aweze kuwatatulia suala hilo ambalo
limechukua muda mrefu wanalofanyiwa na wafugaji hao,ambao bila kujali wamekuwa
wakikata miche hiyo waliyootesha ya mikorosho na kulisha mifugo hiyo kwenye
mashamba wanayotumia kulima.
Alisema kitendo wanachofanyiwa cha kukata mimea na
kulisha mifugo hiyo kwenye mashamba ya wakulima hao, kinaweza kuhatarisha amani
na utulifu uliopo hapa nchini na kusababisha mapigano na mauaji ya kutisha toka
pande zote mbili.
“Hivyo tunamuomba Rais wetu kututatulia suala hili ambalo
linaloonyesha kutoweka kwa amani na utulivu kutokana na vurugu tunazofanyiwa na
wafugaji hao kwa kuwa hata usalama wa wakazi wa kijiji kuwa ni mdogo hivyo
tunahitaji kuishi kwa usalama na sivyo vinginevyo” alisema.
Naye Jackson Makochi (80) mkulima wa kijiji hicho
cha Leganga alisema kuwa serikali isipoingilia kitendo hicho cha wafugaji cha
kuharibu mimea iliyooteshwa na wakulima,kinaweza kutokea mauaji ambayo
yanayoweza kuhatarisha kukosa kuaminiana kati yao na sisi.
Makocho hata hivyo anasikitisha kuwepo kwa ukimia
kuhusu suala hilo ambalo kwa viongozi wa ngazi ya wilaya tayari wameshatarifiwa
kwa ajili ya kulitatua,lakini pia na wao wamekaa bila kulitolea uvumbuzi
wowote.
“Wakulima wa kijiji hicho wanaweza kufikia mahali
wakachoka kutokana na tabia hiyo wanayofanyiwa na jamii hiyo ya wamasai ya
kukatiwa mimea yao mashambani pamoja na kulisha mifugo hiyo kwenye
mashamba,sisi tunataka amani na utulivu na ndiyo maana tunamuomba rais wetu
kutatua suala hili ambalo hivi sasa linazidi kuwa baya” alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya kijiji
hicho cha Leganga Andason Chilingo akizungumza na waandishi habari kijijini
hapo,alikiri kuwepo kwa mgogoro huo kwa muda mrefu kati ya pande zote mbili ya
wakulima na wafugaji wa jamii ya kimasai wanaodaiwa kuharibu mimea mbalimbali
na kuifyeka mikorosho huku mashamba yao wakichungia mifugo.
Alisema tatizo hilo lipo kwa wakazi wa kijiji hicho
ambapo baadhi ya wafungaji wa kimasai wamekuwa na tabia ya kulisha mifugo yao
kwenye mashamba ya wakulima na wakati huo huo wakifyeka miche ya mikorosho
ambayo imepandwa kwa agizo la serikali katika wilaya hii ya Kongwa.
Chilingo alisema kuwa hivi karibuni mkulima mmoja
wa kijiji hicho Mashaka Chiloa alifanyiwa vurugu kwenye shamba lake la hekari
tatu la miche ya mikorosho kwa kuifyeka na huku mifugo yao wakilisha katika
mashamba yao.
“Mimi kama mwenyekiti wa serikali ya kijiji
ninakiri kuwepo kwa tukio hilo ambalo linalofanywa na wafugaji wa kimasai,ambao
hivi karibuni wanifanikisha kukata miche ya mikorosho ya mkulima mmoja na
kusababishia hasara kubwa ya mamilioni ya fedha, hivyo
ninaiomba serikali yetu sikivu kuingilia kati suala hili ili kuepusha uvunjifu
wa amani” alisema.
Mwenyekiti huyo wa serikali ya kijiji alisema kuwa
kutokana na hovu iliyojengeka kati ya pande zote hizi mbili kuna hatari ya
wakazi hao wakashindwa kulima mashamba yao kwa kuofia usalama wao,hivyo
ninaiomba serikali kuchukua hatua za kisheria ili waweze kulimaliza tatizo hilo
kwa amani na utulivu
MWISHO
Comments
Post a Comment