Na. Mwandishi Wetu, DODOMA
SHEKHE Bashart Rehman Butt wa Jumuiya ya kiislamu Tanzania amewaomba viongozi wa madhehebu ya dini kuwahimiza
waumini wao kuwaombea wagombea wa vyama vya siasa watakaochaguliwa ili waweze
kufanya kazi ya maendeleo kwa kushirikiana.
Aidha, maombi hayo pia yaambatane kwa wagombea hao kuwawezesha kuondoa utofauti zao za kiitikadi za vyama vyao vya siasa ili kusudi kila mmoja wake akawajibike kwa malengo ya kuliletea Taifa maendeleo.
Kiongozi huyo wa dini amesema hayo kwenye maadhimisho ya sherehe ya Maulid alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.
Bashart alisema kuwa maombi hayo ni muhimu kwa viongozi hao watakaochaguliwa yatawawezesha pia kuondoa utofauti wao kawa kipindi walichokuwa kwenye mchakmchaka wa uchaguzi.
Hata hivyo Jumuiya hiyo ya Ahmadiyya imewaomba waumini wa dini ya kiislamu kusheherekea sikukuu hiyo ya Maulid kwa kuwakumbuka jamii ya watu wasiojiweza wenye mazingira magumu.
Alisema kuwa moja ya mafundisho ya Mtume Mohamadi ni pamoja na kuwakumbuka watu wasiojiweza,hivyo waumini wenye uwezo wanaombwa pia kuwakumbuka katika kipindi chote.
Mbali ya kusherehekea na jamii hiyo isiyojiweza pia waumini wanatakiwa kuwakumbuka wagonjwa mahosiptalini, wafungwa magerezani na watu wenye ulemavu ambao hawajiwezi kimaisha.
Aidha, amewataka waumini kutekeleza maadili ya kiongozi huyo kwa kuyafanya kwa vitendo ikiwa na kujiepusha na chuki na dharau kwa jamii inayowazunguka.
"Katika kipindi hiki cha sikukuu ya maulidi waumini siyo cha kuadhimishwa kwa kula vyakula na kunywa vivywaji,bali tunatakiwa kutekeleze maafundisho yake kwa ajili ya kujilinda na matendo maovu" alisema.
Alisema kuwa kuna makundi mengi hayana uwezo kwenye vipindi kama hivi vya sherehe,hivyo ni wajibu kwa waumini ambao wana uwezo kuwakumbuka ili na wao waweze kumkumbuka Mtume wao.
MWISHO
Comments
Post a Comment