Na. Mwandishi Wetu,
MGOMBEA
nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi
(CCM), Dkt. John Magufuli ameibuka mshindi kwa zaidi ya asilimia 84 ya kura
zote zilizopigwa.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Rufaa (Mst),
Semistocles Kaijage alipokuwa akitangaza matokeo hayo
katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),
jijini Dar es Salaam.
Jaji Rufaa (Mst), Kaijage
alimtangaza Dkt. John Magufuli wa CCM kuwa mshindi wa nafasi
ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata kura zaidi 12,516,252
sawa na asilimia 84.4. “Kutokana na matokeo haya, namtangaza Dkt. Magufuli wa
CCM, kuwa Rais mteule baada ya kuongoza kwa kupata kura nyingi kuliko wagombea
wenzake” Jaji Rufaa (Mst), Kaijage.
Jaji Rufaa (Mst), Kaijage
aliwataja wagombea wengine na kura zao kwenye mabano kuwa ni Queen Sendiga (ADC
7,627), Twalib Kadege (UPDP 6,194), Hashim Rungwe (CHAUMA 32,878), Mazrui
Khalfan Mohamed (UMD 3,721), Seif Maalim Seif (AAFP 4,635) na Tundu Lissu
(CHADEMA 1,933,271).
Wengine
ni Mutamwega Mugahywa (SAU 14,922), Cecilia Mmanga (Demokrasia Makini 14,556), Maganja
Jeremiah (NCCR Mageuzi 19,969), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF 72,885), Philipo
Fumbo (DP 8,283) na Bernard Membe (ACT-Wazalendo 81,129).
Akiongelea
idadi ya waliojiandikisha kupiga kura, alisema kuwa ni 29,754,699, wakati idadi
ya waliopiga kura ilikuwa 15,091,950 na kati ya hizo kura zilizokataliwa ni
261,755.
MWISHO
Comments
Post a Comment