DAR ES SALAAM.
Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar
es salaam limesema linaendelea kusimamia na kuimarisha ulinzi na usalama wakati
majumuisho ya kura yakiendelea kutangazwa katika majimbo mbalimbali katika jiji
hilo.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Kamanda wa Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na waandishi wa akitembelea vituo vya majumuisho ya kura Ili kuangalia hali ya ulinzi na usalama.
Kamanda Mambosasa amesema mji wa Dar es salaam upo salama hivyo ni vyema wananchi wakaendelea kuwa watulivu na kusubiri kwani matokeo yanatoka baada ya kumalizika kuhesabiwa kwa kura.
Aidha Kamanda Mambosasa amesema wakati wa kampeni umepita hivyo atakaye karibu kuingia barabarani kwa lengo la kufanya vurugu watamchukulia hatua kali za kisheria.
Baada ya watanzania hapo jana kushiriki katika Uchaguzi mkuu kupiga kura kuwachagua wabunge,madiwani pamoja na Rais sasa wametakiwa kuendelea kuwa watulivu wakati matokeo yakiendelea kutangazwa.
Mwisho.
Comments
Post a Comment