Na. Mwandishi Wetu,
Tume ya uchaguzi Zanzibar
imemtangaza Dkt. Hussein Mwinyi kuwa mshindi wa urais Zanzibar kwa kupata ushindi wa 76. 27% baada ya kumshinda mpinzani wake wa Chama cha ACT- Wazalendo Maalim Seif akiwa ni
mshindi wa pili kwa kura 19.87%.
![]() |
Dkt. Hussein Mwinyi |
"Nimepokea ushindi kwa mikono miwili, nashukuru kuwa
wananchi walio wengi wamenichagua mimi na chama changu cha Mapinduzi kwa miaka
mitano ijayo,” alisema
Rais mteule.
Nawashukuru kwa uvumilivu na ustahamilivu mkubwa. Nawashukuru
zaidi kwa kunipigia kura za kutosha kuwa rasi wa Zanzibar. Nitalipa imani hii
kwa utumishi uliotukuka," alisema Dkt. Mwinyi.
Mwinyi ameeleza pia kuwa Zanzibar mpya itajengwa na Wazanzibari
wote bila kujali itikadi, Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofuati hizo.
Rais huyo mteule aliwataka wafuasi wa chama chake kusherehekea kwa ustaarabu
bila ya kukwaza wengine kwa kuwa ushindi wasingepata pasipo kuwa na ushindani.
MWISHO
Comments
Post a Comment