Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Mgombea ubunge wa Jimbo la Dodoma mjini kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Anthony Mavunde ameibuka mshindi katika Jimbo hilo lililopo
ndani ya Jiji la Dodoma.
![]() |
Msimamizi
wa
Uchaguzi Jimbo la Dodoma Mjini, Wakili Msekeni Mkufya akitangaza
matokeo ya Jimbo hilo
Akitangaza matokeo ya uchaguzi jimbo hilo, Msimamizi
wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, Wakili Msekeni Mkufya amemtangaza Anthony
Mavunde kuwa mshindi wa Jimbo la Dodoma Mjini.
Wakili Mkufya alisema kuwa Mavunde alipata kura 86,656 sawa na asilimia 86.44 akifuatiwa na Aisha Madoga wa CHADEMA mwenye kura 13,589 sawa na asilimia 13.50.
Alisema kuwa jumla ya wananchi 335,324 walijiandikisha wakati waliopiga kura ni 102,769.
![]() |
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma Mjini, Wakili Msekeni Mkufya akimkabidhi cheti cha ushindi wa
Jimbo hilo, Antony
Mavunde wa Chama cha Mapinduzi kuwa mshindi wa Ubunge wa Jimbo hilo
MWISHO
Comments
Post a Comment