![]() |
Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Dodoma Philipo Eliamini |
Na Rahim Shaban, Dodoma.
Wafanyabiashara
Mkoani Dodoma wametakiwa kuhakikisha wanalipa kodi ya awamu ya tatu kabla ya kumalizika
septemba 30 mwaka huu ili kuepuka adhabu kutokana na ucheleweshaji wa ulipaji
wa kodi.
Philipo
Eliamini ni Afisa elimu na Huduma kwa mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato
Tanzania TRA Mkoani hapa ,akizungumza leo na Maisha fm kupitia kipindi cha
Maisha Breakfast amewakumbusha wafanya biashara kukamilisha zoezi la ulipaji
kodi kwani mwisho wakulipa kodi ya awamu
ya tatu ni Tarehe 30,mwezi septemba,2020.
‘’Ndugu
wafanyabiashara kama tunavyofahamu sheria yetu ya mapato ianamtaka kila
mfanyabiashara anayepata kipato au kila mtu anayepata kipato kulipa kodi ya
mapato kila mwaka na kama mtakumbuka kila mwaka huwa tunautaratibu wa kufanya
makadirio ya kodi na mara nyingi makadirio haya kwa wale wafanyabiashara
hutumia mwaka wa kalenda kwa maana ya januari mpaka disemba hufanyika kuanzia
mwezi januari mpaka machi na baada ya kufanya makadirio haya huwa tunatoa awamu
nne za ulipaji wa mapato awamu ya kwanza huwa ni mwezi wa tatu ,awamu ya pili
mwezi wa sita na awamu ya tatu huwa ni mwezi septemba na mwisho wa nne huwa ni
mwezi disemba ‘’Philipo
Aidha
philipo amewataka wafanyabiashara hayo kulipa kodi kwa wakati ili serikali
iweze kutekeleza majukumu yake katika kuboresha miundomninu kama vile
elimu,afya pamoja na ulinzi na usalama,huku akiongeza kuwa kushindwa kulipa
kodi kwa wakati kunaweza kusababisha madhara kwa serikali na wafanyabiashara
wenyewe.
‘’unapochelewa kulipa kodi au usipo lipa kodi kimsingi kuna madhara mbalimbali kuna madhari kwako wewe mfanyabiashara lakini pia kwa serikali lakini pia kuna madhari kwa jamii inayokuzunguka’’ Philipo
Sanjari
na hayo Afisa huyo amehitimisha kwa kuwakumbusha waajiri kuwasilisha mapema
kodi wanazokata kutoka kwa wafanyakazi wao,hivyo amewaasa kodi hizo
ziwasilishwe mapema kabla ya tarehe 7, ya mwezi mwingine wa malipo kwa kuwa ni
takwa la kisheria.
‘’TRA
inamtaka kila mwajiri anayezuia kodi hiyo si zaidi ya tarehe saba ya kila mwezi
unaofuata kwa mfano kodi za mishahara ya mwezi tisa ziwasilishwa si zaidi ya
tarehe 7 ya mwezi wa kumi lakini sasa tunasema kwanini usubiri mpaka tarehe
saba kama wewe umeshalipa mshahara kuna baadhi ya waajiri wanalipa mshahara
mapena tarehe 20 ,25,26 sasa kimsingi
zile kodi umewakata wafanyakazi sasa kama umeshazikata tunakusihi uziwasilishe
mapema’’Philipo
Comments
Post a Comment