TAASISI YA HABARI DEVELOPMENT ASSOCIATION YALAANI MATAMSHI YA UCHOCHEZI YANAYOTOLEWA NA BAADHI YA WAGOMBEA KATIKA KAMPENI
![]() |
Mratibu wa Taasisi ya Habari Development Association Hamis Shime akizungumza na waandishi wa Habari katika Mkutano uliofanyika Jijini Tanga. |
Na Jackline Kuwanda, Tanga
Taasisi ya Habari Development Association imelaani
vikali matamshi ya uchochezi yanayotolewa na Baadhi ya wagombea katika kampeni
zao.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Tanga na Mratibu
wa Taasisi hiyo Hamis Shime wakati akizungumza
na waandishi wa Habari Jijini humo.
‘’ Mfano maneno ya mgombea wa Urais Chadema Tundulisu
akiwa kwenye kampeni katika Mikoa mbalimbali Geita,Mara,Mwanza ,Bukoba,Songwe
na wilaya Tarime maneno kama utawala huu ni kizarimu mara oh nimeshinda
uchaguzi mkuu mara tuko kwenye utawala wa hovyo mara tumetawaliwa na kiongozi
muovu jambo ambalo ni baya na ni matusi kwa watanzania watanzania si wote wenye
ushabiki na vyama hivyo ’’ Amesema Shime
Amesema linapokuja suala la kumtukana Rais
aliyepo madarakani na yupo kwenye kampeni siyo kitu kizuri kwani watanzania
walio wengi wanahitaji sera na maono ya nini yatafanyika katika kipindi cha
miaka mitano.
‘’tunalaani matamshi ya aina hiyo na
tunaipongeza hatua iliyochukuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC ya kumuita
tundulisu kwenye kamati ya Taifa ya maadili’’ Amesema Shime
Katika hatua nyingine Shime ametoa wito kwa
vijana maeneo yote nchini kutotumika na
wanasiasa badala yake kuendelea na majukumu yao kama kawaida na siku ya kwenda
kupiga kura basi waende kupiga kwa utulivu.
‘’kwa kuwa wako baadhi ya wanasiasa wanataka
kutuharibia nchi yetu ambayo imetulia ina amani watu wanafanya shughuli zao
vizuri na hakuna bughuza yeyote ile,vijana tutulie tufuate maagizo ya viongozi
wetu ‘’
Kwa upande wake makamu mwenyekiti Taasisi hiyo Issa Omary Chambo amesema kwa sasa vijana wanajitambua kwani hujua ni mgombea yupi anayeeleza sera za kimaendeleo na ni yupi mgombea yupi anaye eneza chuki katika nchi.
‘’kwa hiyo kupitia nyinyi ule ujumbe utakuwa
ni rahisi kuwafikia hawa vijana sidhani kama wapo vijana ambao wanaweza
wakatumika vibaya’’ Amesema Chambo
Naye Benald James Katibu Taasisi hiyo amesema nchi
ya Tanzania ni nchi ambayo haijazoea vurugu matamshi ya kuwagawa watanzania hajiazoeleka
hivyo ni mbaya kwa mgombea yeyote Yule kuacha kunadi sera za chama chake na
ilani yake na kuanza kunadi matamshi ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa nchi.
![]() |
Benald James Katibu wa Taasisi ya Habari Developement Association akizungumza katka mkutano wa waandishi wa Habari uliofanyika Jijini Tanga |
‘’Tunaimani na tunaioyomba tume na vyombo
vingine ambavyo vinasimamia uchaguzi visisite wala kumuonea huruma mtu yeyote
kumchukulia hatua ikiwezekana hata kuzuia asifanye kampeni’’ Amesema James
Hatahivyo wamesema wanaamini uchaguzi wa Mwaka
huu utafanyika kwa amani na zile changamoto ambazo wananchi wanazipitia
zitatatuliwa .
Mwisho
Comments
Post a Comment