Na
Jackline Kuwanda, Dodoma.
Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na shirika
la Afya Duniani WHO 2015 lilitoa taarifa inayoonesha kuwa kila siku Duniani
zaidi ya watoto elfu moja (1000) huzaliwa na sikoseli .
Huku kwa nchi ya Tanzania takwimu zikionesha
kuwa kila mwaka Takribani watoto elfu kumi na moja (11,000) huzaliwa na ugonjwa
wa sikoseli.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na
Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulika na magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dkt James
kiologwe kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
,Jinsia , Wazee na Watoto Prof Abel
Makubi wakati akihitimisha mwezi wa kuelimisha jamii juu ya ugonjwa wa sikoseli
ulioanza Septemba 1 na kumalizika septemba 30,2020.
‘’ Takwimu hizi zinaifanya Tanzania
kuwa nchi ya nne Duniani kuwa na wingi wa ugonjwa wa sikoseli ikiongozwa na Nigeria
ambapo watoto ishirini hadi thelathini kati ya elfu moja wanazaliwa kila mwaka wakiwa na sikoseli’’ Amesema
Amesema hadi sasa Tanzania ina
takribani zaidi ya wagonjwa laki mbili wa sikoseli wanaotambulika kwenye vituo
vya kutolea huduma za Afya huku akisema takwimu zinaonesha kuwa kati ya
watanzania mia moja miongoni mwao 15-20 wanavinasaba vya ugonjwa huo hivyo
wanauwezekanao wa kupata watoto wenye ugonjwa wa sikoseli iwapo watakuwa na wenza wenye vinasaba vya
sikoseli.
‘’tafiti mbalimbali zilizofanywa hapa
nchini zinaonesha kwamba takribani watoto saba kati ya mia moja wenye umri wa
miaka mitano hufariki kutokana na ugonjwa wa sikoseli’’ Amesema
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa
Magonjwa ya ndani kutoka Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam Dkt Elisha
Osati amesema katika kipindi chote cha mwezi wa tisa wameweza kutoa elimu kwa
jamii juu ya ugonjwa wa sikoseli lakini inaonekana kuwa bado kwa nchi ya
Tanzania kunaelewa mdogo kuhusiana na ugonjwa huo.
‘’nchi yetu bado kuna uelewa mdogo
kuhusiana na ugonjwa huu katika kipindi cha mwezi wa tisa tumejitahidi kufanya
mambo megni ikiwemo kutoa elimu kwa jamii kuufahamu zaidi ugonjwa huu na njia
pekee ya mtu kujikinga asipate sikoseli ni kujiepusha kuingia kwenye mahusiano
na mtu mwenye vinasaba vya sikoseli’’ Amesema
Zuhura Makuka ni mama mwenye mtoto
mwenye ugonjwa wa sikoseli amesema watoto wengi wana ugonjwa huo lakani wazazi
hawafahamu kama watoto wana maradhi hayo huku akigusia kuwa kuna hali ya
unyanyapaa kwa watoto wenye ugonjwa huo na wapo pia ambao huusisha ugonjwa huo
na imani za kishirikina.
‘’ukitembelea vituo vya kutolea huduma
za afya ukienda wodini asilimia kubwa ya watoto wana sikoseli ugonjwa huu
lakini haufahamiki na unyanyapaa bado ni mkubwa wanaamini kuwa mtoto
anapozaliwa na ugonjwa huu basi amerogwa’’ Amesema
Mwingine wa wakina mama ambaye ana mtoto mwenye ugonjwa wa sikoseli anaeleza hali
ilivyokuwa wakati bado hajafahamu kuwa mtoto wake ana ugonjwa huo.
‘’ nilianza kuona mwanangu ana kama kiuvimbe
kwenye mkono tukakaa tena siku tatu nikaona tena mkono mwingine ukaanza kuvimba
alikuwa analia sana baada ya kwenda
kituo cha afya cha makole wakanambia
mwanao hana damu wakanambia niende hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma baada
ya kwenda walimpima wakaniambia mtoto wako ana ugonjwa wa sikoseli’’ Amesema
Ugonjwa wa Sikoseli yaani selimundu
hutokana na kurithi kutoka kwa Wazazi wawili yaani Baba .
Hitimisho la mwezi wa kuelimisha jamii
juu ya ugonjwa wa sikoseli ulianza septemba 1 hadi 30 umekwenda sambamba na
kauli mbiu isemayo ‘’Ijue Sikoseli,Epuka Unyanyapaa’’
Comments
Post a Comment