LATRA yatangaza nauli za treni ya abiria Moshi - Arusha

 Na. Mwandishi Wetu,

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza nauli za treni ya abiria itakayofanya safari zake kutoka Moshi mjini hadi Arusha na kurudi Moshi. Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Arusha leo tarehe 29 Septemba, 2020, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe amesema nauli hizo zimetangazwa kufuatia Shirika la Reli Nchini (TRC) kuwasilisha maombi ya nauli hizo, ambapo LATRA ilifanya mikutano ya kupokea maoni ya wadau, kisha kufanya uchambuzi wa maoni hayo pamoja na kuchambua mchanganuo uliowasilishwa na TRC.

Kwa mujibu wa kifungu cha 21 (2) (b) cha Sheria ya LATRA namba 3 ya 2019, baada ya mchakato wa uchambuzi kukamilika, Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA imeidhinisha nauli hizo na kuainisha nauli zitakazotumika kwa usafiri wa treni ndani ya mikoa hiyo na nje ya mikoa kama inavyoonekana katika jedwali.

 

Nauli zilizoidhinishwa na LATRA zikionesha mchanganuo wa vituo vya ndani nan je ya mikoa husika

 

KUTOKA MOSHI KWENDA

Umbali (KM)

NAULI KWA MADARAJA HUSIKA (SHS):

Daraja la tatu

Pili kukaa

1

RUNDUGAI

22

1,000

1,500

2

KIKULETWA

31

1,000

1,500

3

KIA

37

1,000

1,500

4

USA RIVER

62

1,500

2,000

5

TENGERU

65

1,500

2,000

6

CHEKERENI

75

1,500

2,000

7

NJIRO

82

1,500

2,000

8

ARUSHA

86

1,500

2,000

 

 

 

KUTOKA ARUSHA KWENDA

Umbali (KM)

NAULI KWA MADARAJA HUSIKA (SHS):

Daraja la tatu

Pili kukaa

1

NJIRO

4

1,000

1,500

2

CHEKERENI

11

1,000

1,500

3

TENGERU

21

1,000

1,500

4

USA RIVER

24

1,000

1,500

5

KIA

49

1,500

2,000

6

KIKULETWA

55

1,500

2,000

7

RUNDUGAI

64

1,500

2,000

8

MOSHI

86

1,500

2,000

 

Nauli za wanafunzi kutoka mwanzo hadi mwisho wa safari ni Sh. 300.00 kwa daraja la tatu, na Sh 400.00 kwa daraja la pili kukaa.

 

Mkurugenzi Mkuu LATRA Gilliard Ngewe akimkabidhi Henry Machoke, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara TRC andiko la nauli zilizoidhinishwa

 

Wakati huo huo, LATRA imeiagiza TRC kutekeleza masuala mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya usalama kwa wadau husika, kutumia mfumo wa tiketi za kielektroniki, kutoa ratiba za safari kwa umma, kutekeleza hatua za usalama kudhibiti msongamano wa abiria, kuboresha miundombinu na huduma za kijamii, kuweka kitengo cha huduma kwa wateja na kutangaza nauli zilizoidhinishwa katika vyombo mbalimbali vya habari ili ziwafikie wadau wengi zaidi.


Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.