WATOTO 5 WENYE UALBINO WAPEWA MSAADA WENYE THAMANI YA ZAIDI YA LAKI 9

 Na Rhoda Simba, DODOMA 

TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Albinism awereness Foundation (AAF) kwa kushirikiana na Organisation for Social Support Initiatives and Enviroment (OSSIEC) Wametoa msaada wa mahitaji kwa watoto watano wa familia moja wenye Ualbino wanaoishi mtaa wa Kikuyu jijini hapa wenye thamani ya zaidi ya laki 9.

Akiongea kabla ya kukabidhi msaada huo Mkurugenzi wa AAF, Suleiman Magoma amesema aliguswa na kuona anahitajika kusaidia familia hiyo.

"Mara ya kwanza nilipokuja hapa nilikuja na rafiki angu ambae ni Mkurugenzi wa Ossiec, Kennedy Kassian nikaona mazingira wanayoishi nikaamua kuwashirikisha wafanyakazi wenzangu   maana niliona naguswa na nikiwatazama naona wanafanana na mimi" amesema Magoma.

Aidha, msaada huo ni pamoja na kofia,miwani ya jua mafuta kwa ajili ya ngozi cherehani , telescopy kwa ajili ya kutumia kusoma wakiwa mbali na biashara ya genge kwa mama mwenye watoto kwaajili ya kujishughulisha ili aweze kujikwamua kiuchumi.

"Sisi kama Taasisi tutaendelea kufuatilia biashara namna inavyoenda tunakua kama walezi na endapo itakwama tutaendelea kuwapa mawazo," amesema Magoma.

Naye Mkurugenzi wa Ossiec Kennedy Kassian amesema wao waliona kumpa mtu chakula peke yake kwa mara moja haitoshi.

"Unapompa mtu chakula anakula kwa siku moja hujamsaidia bado kwasababu kitaisha sisi tukaona ni bora tutoe kitu ambacho ni tutaweka alama na msingi wa maisha yao "amesema Kennedy.

Kwa upande wake katibu wa Chama cha watu Wenye Ualbino Dodoma (TAS), Hudson Seme amesema kazi kubwa ya TAS ni kufanya ushawishi na utetezi wenye haki kwa watu wote wenye Ualbinism, kutoa elimu ya kiafya na elimu ya kidunia na kuwatambua na kuwaunganisha na fursa mbali mbali zinazojitokeza.

"Kikubwa ni upendo AAF imekua ikijitoa kwa kadri inavyoweza kwa kuhakikisha mtu yoyote mwenye ualibinism haachwi nyuma" amesema Hudson.

Hata hivyo Taasisi ya AAF ilianzishwa mwaka 2016 ikiwa na lengo la kuboresha hali za watu wenye ualibino Nchi.

 

Mwisho

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.