WATENDAJI WAKUU IDARA ZA MAJI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO KUSAIDIA WANANCHI KUPATA MAJI YA UHAKIKA

 

Na Rhoda Simba,Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amewataka watendaji wakuu katika idara za Maji kufanya kazi kwa ushirikiano kwa ajili kusaidia wananchi kupata huduma hiyo kwa uhakika.

Akifungua leo kikao kazi cha kutathimini utendaji kazi katika sekta ya Maji Mhandisi Sanga amesema kuja baadi ya watendaji wanafanya kazi bila ushirikiano hali ambayo inaounguza tija katika kutoa huduma hiyo kwa wananchi.

Ametumia fursa hiyo kuwataka watendaji wote katika Idara za Maji kuimarisha utendaji kazi unaozingatia ushirikiano ili kufikia lengo la kuwahudumia wananchi.

"Maeneo mengi bado kuna umimi,naomba umimi huu tuumalize,tushirikiane katika utendaji wetu kwa ajili ya kufanya kazi yetu owe bora zaidi katika kuwatumikia wananchi." Amesema Mhandisi Santa

Aidha amewataka watendaji hao kila mmoja kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana katika eneo lake .

"Kila mmoja naomba ajiulize maswali matatu je katika eneo langu wananchi wanapata huduma bora ya Maji,kama hawapati kuna mradi gani ninaoutekeleza na hakuna mradi mpango gani upo." Amesema Mhandisi Sanga

Pia amewataka kusimamia miradi ya Maji inayongwa na kuhakikisha inajengwa kwa ubora na kwa thamani ya fedha inayotumuka katika mradi husika.

"Miradi mingi hivi sasa tunaitekeleza kwa fefja za" force account" sasa kama mradi unapaswa kukaa miaka 50 na iwe hivyo siyo mradi unajengwa kwa kutumiabfefha nyingi halafu baada ya muda kidogo unakuwa na nyufa,hii siyo sawa"amesema Katibu Mkuu huyo

Awali akiongea kabla ya kuongea mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Utumishi Dkt Francis Michael amesema watumishi wa Umma nchini hawana budi kuzingatia maadili ya utumishi Wa Umma na kuepuka mihemuko ya Kisiasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28 mwaka huu.

" Tunaelekea kwenye kipindi Cha Uchaguzi lazima tujue majukumu yetu nini sisi Kama watumishi wa umma hilo lazima kila mtumishi kulitambua bila kusahau uwadilifu," amesema Dkt Francis.

Amesema kwenye utumishi wa Umma Kuna sheria na kanuni zinazomkataza mtumishi huyo kufanya ikiwemo kutumia nafasi zao kwa manufaa yao au kupendeea mtu fulani.

Pia mtumishi anatakiwa kulinda ubadhilifu au upotevu wa fedha ni wajibu wenu kusimamia fedha kwa manufaa ya Tasisi na Serikali kwa ujumla.

SIASA

Aidha amesema katika suala zima la siasa watumishi wa Umma wanahaki ya kidemokrasia kuchagua na kuchaguliwa au kuwa mwanacha wa Chama fulani Cha siasa nchini.

Pia amesema mtumishi wa umma kushiriki katika masuala ya siasa katika vyama vyao inaruhudiwa ila tu wasipendelee mtu kwakuwa mtumishi huyo au watumishi hao watakuwa na mapenzi na Chama fulani Cha siasa .

Amesema utakuta mtumishi kwasababu tu anamapenzi na Chama fulani Cha siasa basi anakuwa anatoa  taarifa au nyaraka za Serikali na kupeleka katika Chama fulani Cha siasa huko ni kutoa Siri za Serikali.

" Katika masuala ya siasa mtumishi wa Umma hanabudi kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa za utumishi wa Umma na utawala bora," amesema Dkt Farancis.

Naye Naibu Mwanasheria Mkuu Serikali ,(DAG) Dkt. Evaristo Longopa amesema kila mtu anahaki kikatiba kuchagua na kuchaguliwa na kutoa maoni yao.

Hata hivyo amesema katika ibara ya 20 kwenye katiba yetu inasema raia yoyote anahaki ya kushiriki na wenzake kwenye vikundi vya ushirika au vyama vya siasa.

Amesema ibara ya113 (a) inakataza majaji na mahakimu kujiunga na Chama chochote Cha siasa kwa sababu wenywe ndio watoa haki hivyo hawatakiwi kuwa  wanachama wa Chama Cha siasa.

 

Mwisho

 

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.