Waandishi Mtwara wapigwa msasa kuhusu Corona


 

Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Katika kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa juu ya namna ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko, waandishi wa wa habari mkoani Mtwara wamejengewa uwezo ili kuweza kupeleka taarifa sahihi kwa wananchi hususani wakati huu ambao dunia imekumbwa na ugonjwa wa Covid-19.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo wakati wa kujengewa uwezo, mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa, Sasita Shabani amesema mafunzo hayo yatawasadia na kupeleka taarifa sahihi kwa wananchi namna ya kujikinga na magonjwa hayo na kuchukua tahadhari.

“Naamini kama wanahabari wataendelea na utaratibu huu wa kujengeana uwezo na kukumbusha namna ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko nchi yetu itaendelea kuwa salama na kuwa na Taifa la watu wenye afya njema,”amesema Shabani

Kwa upande wa wanabari wametoa pongezi kwa saasita Shabani kwa mafunzi huku wakiahidi kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu hiyo kupitia vyombo vya vya habari.

Mafunzi hayo yaliandaliwa na Chama cha waandishi wa Habari Mkoani Mtwara (MTPC)  wakiwa na lengo la kuwambusha wanahabari juu majukumu yao ya kuwaelimisha wananchi namna ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.