Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Mgombea uras kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. John
Magufuli kujenga uwanja mkubwa wa michezo Dodoma utakaoweza kubeba wananchi
wengi zaidi kwa wakati mmoja.
![]() |
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli |
Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo katika hotuba yake ya
uzinduzi wa kampeni ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.
“Leo Dodoma imefurika, uwanja wa Jamhuri
umejaa, lakini hata kule nje nako kumejaa. Hii inanipa changamoto kuwa
nitakapochaguliwa kuwa Rais ni lazima nijenge uwanja mkubwa kuliko uliopo na hii
itakuwa ndiyo kazi yangu ya kwanza. Dodoma ni Jiji, na leo mmefunga kazi,
asanteni sana wana Dodoma. Hii inadhihirisha wazi kuwa hapa ni makao makuu ya
nchi” alisema Dkt. Magufuli.
Aidha, aliwataka watanzania kuendelea kumuomba Mungu ili
azidi kuliongoza na kulisimamia Taifa la Tanzania liendelee kuwa na amani na
umoja katika kipindi cha uchaguzi mkuu na baada ya uchaguzi mkuu.
Akimkaribisha mgombea urais kwa tiketi ya CCM, mgombea
mwenza wa chama hicho, Mama Samia Suluhu Hassan, alisema kuwa serikali chini ya
CCM imetekeleza kwa kishindo Ilani ya uchaguzi ya chama hicho. “Ndugu wananchi
niseme, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tumeweza kutekeleza kwa kishindo
na tumeweza…Twende tukasonge mbele katika kampeni kwa heshima na kuomba kura
kwa wananchi. Tukafanye kampeni kwa amani na kupiga kura kwa kishindo, tupate
maeneldeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii” alisema Mama Samia.
Chama cha Mapinduzi kimezindua kampeni kuelekea
uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani katika uwanja wa Jamhuri jijini hap
ana zitaendelea nchi nzima kwa takribani miezi miwili.
MWISHO
Comments
Post a Comment