![]() |
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodom, Mustapher Shaaban akitoa hotuba ya Swala ya Eid katika Msikiti wa Gadafi Jijini Dodoma baada ya swala ya Eid. |
Na Majid Abulkarim, Dodoma.
Waumini wa Dini ya
Kislamu nchini wametakiwa kuliombea taifa kudumisha amani na utulivu uliyopo
hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu utakao fanyika 28 Oktoba
2020 ili kuweza kupata viongozi bora , waadilifu na wazalendo katika
kuwatumikia watanzania kwa kuleta maendeleo.
Wito huo umetolewa
na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodom, Mustapher Shaaban katika Msikiti wa Gadafi
Jijini Dodoma wakati wa swala ya Eid.
Sheikh Shaaban
amesema kila mtanzania anawajibu wa kuliombe taifa ili kuhakikisha linalinda
amani na utulivu katika kuelekea Uchanguzi Mkuu ili viongozi watakao
patikana kutokana na maombi ya watanzania wakasimamie katika kuleta
maendeleo ya taifa .
“Hivyo maombi hayo
yatasaidia kupata viongoz waadilifu, wema , wanyenyekevu ,wanao
sikiliza wananchi wao, wenye uzalendo na kutatua kero za watanzania kwa
wakati bila kuleta uvunjifu wa amani na mshikamano uliopo katika nchi yetu”,
ameeleza Sheikh Shaaban.
Mbali na hilo
Sheikh Shaaban amesema dini ya uislam inafundisha amani na mshikamano
hivyo ni vema kupeana ushirikiano kwa ustawi wa amani na maendeleo nchini
ili kujenga taifa bora.
Aidha Sheikh
Shaabani amewataka wamini hao kutumia siku ya Eid kuwaombea ndugu na marafiki
wote waliyotangulia mbele za haki kusamehewa makosa yao yote kwa Mwenyezi Mungu
na kusema mambo mazuri juu yao ili kupata kauli thabit kwa Allah.
Pia Sheikh Shaabani
amekumbushia kuwa leo ndo siku muhimu watu wanatakiwa kukaa na familia zao kwa
kujumuika na kufanya ibada, ya kuchinja kwa wale wenye uwezo wa kuchinja na
kutoa sadaka kwa watu wasio kuwa nauwezo ili kutimiza adhima ya siku kuu ya
Eid.
Sheikh Shaabani
amemaliza kwa kutoa pole kwa Taifa kwa kumpoteza Hayati Benjamini Mkapa
aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu na kusema kuwa waumini wa Dini ya Kislamu
watamuenzi kwa mambo mengi ikiwemo Ujenzi wa Msikiti wa Gadafi ulijengwa
kipindi cha Utawala wake na kipindi hicho aliyatoa majengo ya kilichokuwa
Chuo cha ufundi cha TANESCO Mkoani Morogoro kutumika kuanzisha Chuo Kikuu cha
Waislamu cha Morogoro mnamo mwaka 2004.
“Hivyo waumini
tunamuenzi Hayati Mkapa kwa hayo mambo mawili makubwa kwani leo tumepata ibada
yetu ya swala ya Eid hapa na watoto wetu wanaendelea kupata elimu Chuoni hapo
na wanapomaliza masomo yao wanapata ajira na kulitumikia taifa”, ameweka wazi
Sheikh Shaaban.
Comments
Post a Comment