WANAFUNZI ZAIDI YA 20 SHULE YA SEKONDARI KATUMBA WILAYANI MPANDA WAFUKUZWA SHULE,WAZAZI WASHINDWA KUMUDU MICHANGO
Na. Mwandishi Wetu, MPANDA
Wanafunzi zaidi ya 20 wa Kidato cha nne Katika
shule ya Sekondari Katumba iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi
wamefukuzwa shuleni na kupewa adhabu ya kufyatua tofari 300 kila mmoja ikiwa ni
adhabu ya kutoishi Bwenini kama mkakati wa shule hiyo.
Mpanda Redio FM imezungumza na Wazazi na walezi wa
baadhi ya wanafunzi hao ambao wamesema wameshindwa kumudu michango ya chakula
inayofikia kiasi cha elfu 65 na kwamba adhabu hiyo imetolewa wakati wanafunzi
wengine wakiendelea na mitihani ya kujipima .
Tumemtafuta Mkuu wa shule hiyo bila mafanikio ,
Lakini Mpanda Redio fm
inafanya jitihada za kumtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo pia .
Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Tanzania akiwa
mkoani Katavi kwajili uzinduzi wa ujunzi wa Bandari ya Kalema aliagiza wakuu wa
shule kuacha kufukuza wanafunzi kwaajili ya michango badala yake waache
wanafunzi waendelee na Masomo.
Chanzo Mpanda Redio FM
Comments
Post a Comment