TRC KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA SERIKALI NA BINAFSI


Na. Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

Shirika la Reli Tanzania-TRC limesema kuwa   limeazimia kushirikiana kwa ukaribu na asasi za serikali na binafsi ili kuhakikisha jamii inayoishi pembezoni mwa reli zinafaidika na ujio wa miradi inayisimamiwa na TRC wakati wa ujenzi, na mara  baada ya ujenzi na uboreshaji wa reli ya kati inayotoka mkoa wa dar es salaam hadi isaka.

Akizungumza jana  jijini Dar es salaam mara baada ya TRC na Taasisi hizo kusaini mikataba ya utekelezaji wa mikakati mbalimbali ili kuboresha maisha ya jamii zinazoishi pembezoni mwa reli, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Amina Lumuli amesema mikakati ya kuboresha jamii hizo imetokana na matokeo ya kazi kubwa inayofanywa na serikali kwa kufanya maamuzi ya kuimarisha sekta ya miundombinu ya reli nchini ikiwa ni pamoja na  kujenga reli yenye kiwango cha kimataifa -SGR, Kuboresha reli ya kati pamoja na kufufua njia mbalimbali za reli.

Aidha, amebainisha kuwa shirika la reli linatambua umuhimu na mchango unaotolewa na taasisi binafsi na za serikali kwa jamii hivyo TRC itaendelea kuongeza nguvu na ushirikiano kwa taasisi hizo ili kuleta matokeo chanya katika utekelezaji wa miradi nchini.

Kwa upande wake Meneja miradi wa ujenzi wa Reli ya SGR anayehusika na ujenzi kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro Machibia Masanja amesema kuwa uwepo wa ujenzi wa mradi huo utakuwa na manufaa kuanzia ujenzi wake mpaka kuendelea kutumika

MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.