MAOFISA MIPANGO MIJI WATAKIWA KUACHA TABIA YA KUACHIA KAMPUNI BINAFSI KURASIMISHA ARDHI KATIKA MAENEO BILA KUWA NA USIMAMIZI WAO
Na.
Mwandishi Wetu, DODOMA
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika amewataja maofisa mipango miji kuwa chanzo cha
ujenzi holela ambao umekuwa ukijitokeza katika maeneo mbalimbali kwani
hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.
Akizungumza jijini hapa jana kwenye mafunzo
ya siku mbili ya maofisa mipango miji wa Mikoa na Makao makuu ya Wizara ya
Ardhi, kwa niaba ya Katibu Mkuuu, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wizara hiyo, Ezekiel
Mpanda amesema maofisa hao wamekuwa wakilalamikiwa kila sehemu kutokana na
utendaji wao wa kazi.
Mpanda amesema maofisa hao hawatoi elimu
kwa wananchi ili wajue sheria za adhi na kawaacha wajenge holela, hali ambayo
inasababisha wengi kubomolewa nyuma zao na kuingia hasara.
Hata hivyo amewataka maofisi hao kuacha
tabia ya kuwaachia kazi kampuni binafsi kurasimisha maeneo bila kuwa na
usimamizi wao kwani baadhi yao wamekuwa wakishindwa kukamilisha kazi waliyopewa
kwa wakati.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa
Wataalam wa Mipango Miji, Prof. Wilbard Kombe amesema
Maofisa hao licha ya kazi wanazozifanya lakini baadhi yao wamekuwa si waaminifu
kwani wanafanyakazi na kampuni ambazo hazijasajiliwa.
Akizungumzia utafiti walioufanya hivi
karibuni kuhusu Mipango Miji, mkuu wa Shule kuu ya Mipango Miji katika
Chuo Kikuu cha Ardhi, Dk Ally Namangaya amesema utafiti huo ulilenga kujua
kwanini utekelezaji wa mipango miji ni mdogo katika maeneo mbalimbali nchini
huku Ofisa Mipango Miji mkoani Geita, Oscar Yohana akieleleza jisni watakavyokabiliana na changamoto
hizo.
MWISHO
Comments
Post a Comment