Na. Mwandishi Wetu, DODOMA
KUTOKANA na kupungua kwa hali ya maambukizi ya ugonjwa wa
Covid-19 nchini Jeshi la Magereza limelegeza masharti ya katazo la
kutokutembelea wafungwa na mahabusu ambapo kuanzia Agosti 1 mwaka huu huduma ya
kutembelea wafungwa/mahabusu kwa huduma mbalimbali magerezani zimerejeshwa.
![]() |
SSP Amina Kavirondo |
Akizungumza na
waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma Msemaji wa Jeshi la Magereza, SSP Amina
Kavirondo amesema kuwa kufuatia kuripotiwa uwepo wa ugonjwa wa Corona nchini
jeshi la magereza lilisitisha huduma zote za kutembelea wafungwa na mahabusu
ikiwemo huduma za kupelekewa chakula.
“Hatua hii imekuja
baada ya kushuka kwa kasi ya maambukizi Tanzania kwa kiasi cha kuridhisha na
kwa kuzingatia tamko la Rais John Magufuli la kuzitaka taasisi mbalimbali za
serikali kurejea katika shughuli za awali za utendaji kazi” amesema.
Amesema kuwa
Jeshi la Magereza linawataka wageni wote pamoja na kuzingatia sheria,kanuni na
miongozo ya jeshi na wizara ya afya wakati wa upokeaji wa huduma hiyo.
Wakati huohuo, alisema kuwa
wageni watatakiwa kuzingatia mambo muhimu yafuatayo,mfungwa/mahabusu
atatembelewa na ndugu wasiozidi wawili tu kati ya jumamosi au
jumapili,mazungumzo yatatakiwa yasizidi dakika tano,na wenye vibali vya kuleta
chakula italazimika kuletwa na mtu mmoja tu.
“Mambo mengine
ni pamoja na wageni wote wavae barakoa na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni
wanapoingia eneo la Gereza na wanapongia gerezani,kuwa umbali wa mita moja kati
ya mfungwa/mahabusu na mgeni lazima uzingatiwe na mazungumzo ya kisheria
kati ya wakili na mteja wake yasizidi saa moja” alisema Kavirondo.
MWISHO
Comments
Post a Comment