Na. Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
Chama cha Siasa cha
Aliance for Democratic Change (ADC) kimesema mpaka sasa kimetoa fomu
za Ubunge 36, wawakilishi 32, pamoja na Madiwani 76 mkoa wa
Dar es salaam wengi wakiwa ni wanawake wanaotaraji kupeperusha bendera ya chama
hicho katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es
salaam na Naibu Katibu wa Chama hicho, Queen Cuthbeti Sendiga
wakati akifanya mahojiano maalum na kituo hiki akieleza namna wanavyoendesha
mchakato wa uchukuaji wa fomu za wagombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia
chama hicho.
Naibu Katibu huyo wa ADC ambaye pia ndiye
Mgombea Urais wa Tanzania Bara kwa chama hicho amesema chama chao kimepata
muamko wa wanawake wengi kujitokeza kuchukua fomu ili kupata nafasi ya kugombea
Ubunge pamoja na Udiwani kupitia chama hicho.
Aidha, ameziomba
Taasisi zote zinazojihusisha na kuwawezesha wakina mama kusimamia katika
uongozi ni vyema zikaonyesha mchango katika kuwapa mbinu na jitihada wanawake
katika Kupambana kwenye uchaguzi ili kuibuka vinara wa ushindi.
Naibu katika huyo amewahamasisha watanzania
kusimama vyema katika kuilinda na kuitunza amani ya nchi ili uchaguzi huo uweze
kufanyika kwa utulivu na kumpata kiongozi bora.
Hata hivyo Chama hicho cha Aliance
Democratic Change ADC kimesha fanya uchaguzi na kuwateua viongozi wakubwa wa
nchi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano na Mwenza pamoja na mgombea wa Urais
serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
MWISHO
Comments
Post a Comment