RC MAKONDA AZIDI KUWANYIMA USINGIZI WAPINZANI DAR, AKABIDHI MIRADI ILIYOTEKELEZWA NA SERIKALI YA RAIS MAGUFULI KUPITIA ILANI YA CCM
Na. Mwandishi Wetu,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Paul Makonda leo ameendelea na ziara yake ya kukabidhi miradi
Mbalimbali iliyotekelezwa na serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais, Dkt. John
Magufuli kwa Chama cha Mapinduzi CCM na kuwahimiza Wananchi kuchagua Viongozi
wanaoweza kutatua kero zao.
Miongoni mwa Miradi aliyoikabidhi RC Makonda iliyotekelezwa kupitia
Ilani ya CCM kwa upande wa Jimbo la Kinondoni ni Mradi wa Soko la Magomeni
lenye thamani ya Shilingi Bilioni 8.9, Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto
hospitali ya Mwananyamala inayogharimu Bilioni 3 na Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja
Cha Mpira Mwenge chenye thamani ya Shilingi Bilioni 4.5.
Aidha, RC Makonda
pia amekabidhi Mradi wa Ujenzi Barabara ya Morocco hadi Mwenge yenye
thamani ya Bilioni 69.7, Mradi wa Kituo cha Mabasi Mwenge Bilioni 2.5 na Kituo
cha Afya Kigogo chenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.5.
Kesho Jumatano RC Makonda ataendelea na ziara yake kwenye Jimbo la
Kibamba ambapo atakabidhi miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Chama cha
Mapinduzi CCM.
MWISHO
Comments
Post a Comment