Na.WAMJW,DSM
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
imetakiwa kutatua malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa
wananchi wenye bima ya afya.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kikao na
Menejimenti ya Mfuko huo katika ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini, Dar es
Salaam.
“Kumekuwepo na malalamiko ya upatikanaji
wa baadhi ya dawa na vipimo kwa watu wenye kadi za bima pia ucheleweshaji wa
malipo ya watoa huduma za afya" Alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy ameutaka mfuko huo
kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na
mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa katika vifurushi vya bima ya
afya.
"Tatueni malalamiko yote kwa wakati
ili wananchi wafurahie vifurushi vyote watakavyojiunga navyo".Alisisitiza
Waziri Ummy
Kikao hicho pia kiliangalia mwenendo wa utoaji
wa huduma za bima za afya zinazotolewa na mfuko huo ambapo kilihudhuriwa
na Mkurugenzi Mtendaji wa NHIF, Benard Konga, Mkurugenzi wa Tiba kutoka
Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, na Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi.
Comments
Post a Comment