![]() |
Rasi wa Ndai ya Taaluma za Biashara na Sheria Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM Adam Mwakalobo |
Na Jackline Kuwanda, Dodoma.
Rasi
wa Ndaki ya Taaluma za Biashara na Sheria Chuo kikuu cha Dodoma UDOM Adam
Mwakalobo amefungua Warsha ya Mafunzo ya uhuru wa kujieleza kwa wanataaluma wa ndaki ya Taaluma ya Biashara na Sheria Chuoni
humo.
Akizungumza
leo na Waandishi wa Habari mara baada ya kufungua mafunzo hayo amesema mafunzo
yatakuwa ni endelevu kwasababu mwalimu muda wote anapaswa kupata mbinu mpya na
vitu vipya kwani kila siku kumekuwa na mabadiliko mapya .
‘’unajua
mabadiliko kila siku yanabadilika na kunavitu ambavyo vinaingia kwahiyo ni
lazima tupate mbinu mpya za kufundisha
na kujifunza huwezi kukaa tu muda wote lazima upate vitu vipya na uongeze ujuzi
kila wakati kwasababu ya haya mabadiliko yanayoendelea ndiyo maana ya haya
mafunzo ‘’Mwakalobo
Amezungumzia
pia kwa upande tafiti ambapo amesema
kuwa chuo kimetenga fungu maalumu kwaajili ya kuweza kuwasaidia
wanataaluma wachanga wanaochipukia.
‘’ Chuo
kinawasadia wanataaluma wachanga waweze kuomba zile hela yaani ni mashindano na
wakipata wanaenda kufanya tafiti mbalimbali kulingana na maeneo yao ingawa sio
kitu kikubwa sana lakini ni kuwawezesha ili waweze kujiendeleza ,kwasababu
unajua kuandika machapisho na kwenda kushindana ni lazima uwe umejifunza namna ya kuandika andiko’’Mwakaobo
Daktari
Ines Kajiru ni Mkuu wa Idara ya Sheria Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM amesema sio
mara ya kwanza kufanya mafunzo kama hayo wamekuwa wakifanya mafunzo mbalimbali ikiwemo
masuala ya kisheria huku akizungumzia kwa upande wa wanafaika wa mafunzo hayo .
‘’watu
ni wengi wanaonufaika katika mafunzo kama haya nitolee mfano hapa leo watakao
nufaika ni walimu wanataaluma wote wa ndaki ya Taaluma za Biashara na sheria wa
chuo kikuu cha Dodoma’’Kajiru
‘’
Tunacholenga ni kuendelea kukuza uelewa na kuwasaidia wanataaluma kuwajengea
uwezo zaidi wa mambo mbalimbali kuhusu elimu na vilevile uhuru wa kujieleza na
uhuru wa elimu’’ Kajiri
![]() |
Mwalimu Idara ya Sheria Chuo cha Dodoma UDOM Nicodemas Husena |
Naye
mwalimu katika Idara ya Sheria chuoni
humo Nicodemas Husena amesema mafunzo kama hayo yanaongeza uelewa juu ya dhana
nzima ya uhuru wa kujieleza.
‘’kwasababu
kisheria ukisema uhuru wa kujieleza kuna mipaka, kuna haki unavitu huwezi
kusema licha ya kuwa unauhuru wa kujieleza ,lakini vilevile kunavitu unaweza
ukavisema lakini kwa mipaka fulani’’
‘’kwa
mfano sisi Tanzania tuna sheria ya takwimu ambayo inazuia baadhi ya mambo
kwahiyo mafunzo kama haya yanawafundisha washiriki wajue mipaka ya uhuru wa
kujieleza lakini wajue ni yapi ambayo yanaweza yakazuiwa ‘’
Mafunzo
hayo yamefanyika kwa ushirikiano wa Umoja wa Vituo vinavyotoa msaada wa
kisheria wa vyuo vikuu Afrika Mashariki.
Comments
Post a Comment