WANAOJIHUSISHA KIMAPENZI NA WANAFUNZI MKOANI NJOMBE KUWAJIBISHWA


NJOMBE.

Wazazi na walezi kata ya Ibumi wilayani Ludewa Mkoani Njombe wameiomba serikali kuwawajibisha wale wote wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi ili kunusuru wimbi kubwa la matokeo hasi pindi shule zitakapofungua mara baada ya ugonjwa wa Corona kuisha.

Wakizungumza katika mkutano wa Diwani wa kata ya Ibumi Mh,Edward Haule wananchi wamesema kuwa suala la kuleana katika jambo hilo ni kupeana kilema.

Akielezea juu ya ombi la mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Mussa mkatakulima Diwani wa kata ya Ibumi na Mwenyekiti wa Halmashauri  ya wilaya ya Ludewa  Mh,Edward Haule  amesema hatua inatakiwa kuchukuliwa kama ambavyo sheria inasema.


Hata hivyo diwani wa kata hiyo ya Ibumi ametoa wito kwa kuwataka viongozi wa ngazi zote wilayani humo kuhakikisha wanakuwa makini na wanafunzi kipindi hiki cha likizo ya ugonjwa wa Corona na kuendelea.


Felix Charle ni afisa mtendaji kata ya Ibumi na Charles Shadrack Luoga ni afisa mtendaji kijiji cha Ibumi kwa pamoja wameahidi kutekeleza maagizo ya wananchi  pamoja na kiongozi wa halmashauri hiyo



Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.