Wananchi mkoani Njombe wamjia juu mtendaji wa kijiji kwa kuuza eneo lililotengwa kwaajili ya ufugaji wa kilimo
Na. Mwandishi Wetu, NJOMBE
Wananchi wa vijiji vya kata ya Itulahumba
halmashauri ya wilaya ya wangingombe mkoani Nombe kwa pamoja wamepinga kitendo
kinachofanywa na baadhi ya wananchi wenzao kwa kushirikiana na mtendaji wa
kijiji hicho cha kuuza eneo ambalo limetengwa kijijini hapo kwaajili ya ufugaji
na kilimo.
Eneo hilo lenye ukubwa wa zaidi ekari 80 ambalo limeanza kukatwa miti na kulimwa bila makubaliano ya kamati za vijiji pamoja na mkutano wa hadhara wa wananchi hao akiwemo Yohana Mgute na Mary Mwakajuba wamesema serikali isaidie waliovamia kukamatwa na kuzuia uharibifu unaoendelea.
Mtendaji wa kijiji hicho Rudlof Mbilo
anasema eneo hilo licha ya kuwa limetengwa kwajili ya shughuli za kilimo na
ufugaji lakini hakuna nyaraka zinazothibitisha na ndio sababu amekuwa
akiidhinisha watu kuuziana ardhi hiyo.
viongozi wa kata hiyo wakiongozwa na Diwani, Thobias Mkane na Betty Mangula Afisa Mtendaji
wa Kata Hiyo wamepiga marufuku mtu yeyote kufanya shughuli katika eneo
hilo wakati uchunguzi wa kuwabaini waliovamia na kuuza ukiendelea.
MWISHO
Comments
Post a Comment