Na. Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
Wakuu wa vyuo pamoja na shule nchini
wametakiwa kutokuingilia uhuru wa kufanya ibada kwa wanafunzi pindi ambapo
wanarejea mashuleni baada ya kupungua kwa kasi ya maambukizi ya virusi vya
Corona.
Hayo yameelezwa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa
la Waadventista wasabato, Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania, Askofu Mark
Maleleana wakati akikabidhi vifaa kinga kwa hospital za Wilaya ya Temeke ili
kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Askofu Malekela amesema kuwa nchi imefikia
hapa kutokana na maombi yaliyoongozwa na Rais Magufuli hivyo wanafunzi wapatiwe
muda wa kufanya ibada.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mganga
Mkuu wa hospitali ya Temeke, Bi. Grace Ntangu amesema kuwa vifaa kinga hivyo vitatumika kwa
makususi yaliyokusudiwa .
Comments
Post a Comment