Na. Mwandishi Wetu, SIMIYU
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka
amewaagiza Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri zote sita mkoani humo,
kuhakikisha wanalipa stahiki za madiwani kabla ya mabaraza ya madiwani kuvunjwa
wiki tatu zijazo.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka,
ametoa agizo hilo katika baraza maalumu la madiwa wa Halmasahauri ya Wilaya ya
Busega, kwa ajili ya kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za
serikali CAG.
Katika hatua nyinge, Mtaka ameitaka
Halmashauri ya Wilaya ya Busega kuweka mkazo katika ukusanyaji mapato, kutokana
na kukusanya chini ya kiwango, ambapo kwa sasa inakusanya asilimia 45 pekee.
Kauli hiyo imeungwa mkono na Madiwani wa
Halmashauri hiyo, wakisema pamoja na kupata hati safii, suala la kuongeza
ukusanyaji mapato ni muhimu ili Halmashauri iweze kujiendesha na kuhudumia
wananchi.
Kwa upande wake Mbunge wa Busega, Dkt.
Raphael Chegeni, amesema ukusanyaji mapato ni muhimu, hasa ikizingatiwa kwamba
bado kunahitajika ujenzi wa miundombinu ya madarasa ili kutosheleza mahitaji ya
wanafunzi hususan wanaojiunga na elimu ya sekondari.
MWISHO
Comments
Post a Comment