Na. Amiri Kilagalila, NJOMBE
Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya
wakulima inayopelekea kukuwa kwa sekta ya kilimo na kusaidia kuongezeka kwa
pato la mkulima na Taifa, kituo cha utafiti wa kilimo (TARI) Uyole, wanasema lengo
la kituo kwa sasa ni kuona mkulima mahiri na anayefanikiwa
katika maisha kutokana na kilimo bora na chenye tija.
Amebainisha hilo Dkt. Tulole Lugendo
Bucheyeki mkurugenzi wa kituo cha TARI Uyole,wakati akikagua maendeleo ya
shamba la mkulima wa Mahindi kupitia mradi wa kuboresha kilimo na maisha ya
mkulima kwa kutumia mbegu bora lililopo kijiji cha Ilunda kata ya Mtwango
wilayani Njombe.
Vilevile, amesema kwa
sasa kituo cha Uyole kina aina zaidi ya 8 ya Mahindi zitakazomuwezesha mkulima
wa sehemu mbali mbali nchini kufaidika yatakapotunzwa,huku akibainisha kuwa
awali walikuwa na mbegu kwa ajili Nyanda za juu kusini tofauti na
sasa.
Lornad Sabula ni mtafiti kutoka taasisi ya
utafiti wa kilimo Tanzania kituo cha Uyole na meneja wa mradi wa Pata
Tija,anasema kwa sasa wanahitaji kubadilisha mtazamo wa kilimo kwa wakulima
zaidi ya laki moja katika mazao ya Mahindi, Maharage na Soya.
Jafari Mbogela na Anna Wikichi ni wakulima
wa kijiji cha Ilunda wanasema wamepata mafanikio makubwa katika kilimo kutokana
na matumizi ya Mbegu bora za kilimo kutoka kituo cha utafiti TARI, hali ambayo
imewawezesha kupata zaidi ya gunia 50 za mahindi kwa ekari moja tofauti na
awali.
Mpaka sasa mradi wa kuboresha kilimo na
maisha ya wakulima umefanikiwa kuwafika wakulima elfu hamsini wa moja kwa moja
katika mikoa ya nyanda za juu kusini, huku wengine wakifikiwa kupitia kwa wagani, maonyesho ya
kilimo pamoja vyombo vya Habari .
MWISHO
Comments
Post a Comment