Wadau wapambana kuvunja tamaduni ya usiri wa hedhi kwa wasichana katika jamii


Na Amiri Kilagalila, Njombe.

Jamii nchini imetakiwa kuvunja tamaduni ya usiri na kuona  hedhi ni kitu cha kawaida kwa watoto wa kike hali itakayowafanya wasichana kujiamini na kujivunia wanapokuwa hedhi.

Hayo yamebainishwa na kiongozi mkuu wa mradi kutoka shirika la hamble unemployment solution in tanzania Faraja Eliezer ambaye ni mkuu wa idara ya afya na mazingira kutoka shirika hilo,walipofika kituo cha kulea watoto yatima cha Familia ya Upendo Uwemba kilichopo  kijiji cha uwemba kwa ajili ya kutoa elimu juu ya hedhi salama.

Amesema lengo la kufika katika kituo hiki ni kutoa elimu ya hedhi salama kwa watoto wa kike ambao ni yatima,kwani jamii imekuwa ikijitenga kutoa elimu hii kutokana na sababu za kiutamaduni

May 28 huwa ni siku  hedhi Duniani Kabula Kidai msaidizi katika programu maalumu ya Days For Girls Njombe inayohusika na utengenezaji wa Taulo za kike,anasema wamejipanga vizuri kuelimisha watoto wa kike juu ya hedhi salama na kuwataka watoto wa kike kujiamini pindi waonapoona dalili ya hedhi na wasisite kuwaambia walezi wao juu ya hali hiyo.

Mlezi wa kituo cha kulea watoto yatima cha familia ya upendo uwemba Jenifa Msigwa pamoja na watoto wanaoishi kituoni hapa akiwemo Agness Mtewele wanashukuru kwa msaada na elimu waliyopata juu ya Hedhi salama

Siku ya Hedhi Duniani huadhimishwa kila mwaka mnamo tarehe 28-5 ambapo taasisi ya Days For Girls Njombe licha za kutoa Taulo za kike kwa wasichana wamekabidhi barakoa kwaajili ya kujikinga na virusi vya Corona.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.