Uhaba wa walimu wenye sifa za kufundishia watajwa kuwa changamoto ya kutoa elimu kwa watoto wenye umri chini ya miaka sita


DAR ES SALAAM.

Uhaba wa walimu wenye sifa na mbinu rafiki za kufundisha madarasa ya elimu ya awali nchini umetajwa kuwa changamoto ya kutoa elimu kwa watoto walio na umri chini ya miaka sita hali inayokwamisha kuwapatia watoto hao maarifa na malezi kulingana na umri wao.

Hayo yamebainika katika uzinduzi wa matokeo ya tafiti mbili zilizofanywa na shirika lisilo la kiserikali la HAKI ELIMU zilizoangazia makuzi ya mtoto, ulinzi na maendeleo ya elimu ya awali nchini.

Akizungumza katika unzinduzi huo,mkurugenzi mtendaji wa HAKI ELIMU Dkt. John Kalage amesema taifa limepiga hatua nzuri katika sekta ya elimu lakini ameisisitiza jamii kuungana kutatua changamoto zilizopo ili kuwawezesha watoto kupata elimu bora.

Adhabu zilizozidi kipimo ikiwemo viboko na vitisho kutoka kwa walimu vimetajwa katika utafiti huo kama kikwazo cha watoto kujifunza kutokana na kuzua hofu kwa watoto wawapo darasani.

Baadhi ya walioshiriki uzinduzi wa tafiti hizo wameeleza namna bora ya kushughulikia changamoto zilizoanishwa kwenye utafiti katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Tafiti hizo mbili zimefanyika katika wilaya tisa za Tanzania Bara ambapo uzinduzi wake umewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya elimu kwa njia ya mtandao kujadili na kupata ufumbuzi wa changamoto zilizobainishwa katika tafiti hizo.



Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.