RAIS MHE. DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MARAIS WASTAAFU WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI ZA IKULU YA CHAMWINO MKOANI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo la Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika Chepe ili kuweka zege na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi Ujenzi Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 30 Mei 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 30 Mei 2020


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere kuashiria uzinduzi wa Mitambo na magari yatakayotumika katika ujenzi wa Ujenzi Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 30 Mei 2020

Picha zote na Blog ya Ikulu



Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.