Plan International kushughulika na usafiri wa mazingira ili kuhakikisha jamii zinabadili tabia katika masuala ya usafi wa mazingira
Na.
Jackline Kuwanda, DODOMA
Rachel Steven kutoka Shirika la
Plan International amesema kuwa wamekuwa wakishughulika na mradi wa
usafi wa mazingira Tanzania lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa jamii zinabadili
tabia katika masuala ya usafi wa mazingira kwa ujumla wake kuanzia ujenzi wa vyoo
bora, matumzi ya vyoo bora,unawaji wa
mikono ,masuala ya hedhi salama kwa watoto wa kike pamoja na wanawake kwa
ujumla.
Akizungumza na Mtandao wa Dodoma News
katika Siku ya Hedhi Duniani ambayo huadhimishwa Mei 28 ya kila
mwaka.
Rachel amezungumzia hali ya mila, tamaduni ambazo
zimechangia suala la hedhi kutozungumziwa kwa wazi na kusababisha watoto wa
kike kukosa masomo kipindi ambacho wako katika hedhi.
Amesema kuwa watoto wa kike wamekuwa
wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokuwa na miundombinu
rafiki ambayo wangeweza kujisitiri vyema pindi wakiwa mashuleni.
Wakati huohuo, amesema kuwa
mara nyingi watoto wanaokosa masomo wakati wa hedhi ni wale ambao wako katika
shule za msingi.
kutokana na hali hiyo pia amesema kuwa baadhi
ya wazazi wanachangia kwa kiasi kikubwa kwani wengine hufikia hatua ya
kumuombea mtoto ruhusa kwa kisingizio kuwa anaumwa.
Siku ya hedhi salama duniani iliasisiwa na taasisi ya
Kijerumani ya WASH United mwaka 2012 na 2013 waliendesha rasmi kampeni ya #MENSTRAVAGANZA katika mtandao wa Twitter kwa siku 28.
Malengo ya kampeni ilikuwa ni kuongeza ufahamu wa hedhi
salama duniani na uwajibikaji kwa serikali katika kuzitatua changamoto za hedhi.
Mwaka 2014 kampeni ilianza kupata nguvu kutoka mataifa
mbalimbali duniani kupitia kauli mbiu tofauti kwa kila mwaka.
MWISHO
Comments
Post a Comment