Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aharisha kikao cha Bara za madiwani kisa



 MOROGORO.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amelazimika kufikia uamuzi wa kuahirisha kikao cha Baraza maalum la Madiwani cha kujadili taarifa ya Mkaguzi wa hesabu za serikali katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro baada ya kubaini mkanganyiko wa taarifa katika idara ya Fedha na Maendeleo ya Jamii zinazo onyesha kukinzana na uhalisia.

Hoja ya kuahirisha kikao cha baraza la madiwani inakuja baada ya kuibuka utata wa taarifa, katika idara mbili za Fedha na maendeleo ya jamii, ambapo kwa upande wa idara ya fedha afisa mapato wa halmashauri hiyo Joseph Komba alitokomea kusiko julikana, mkuu wake wa idara akisema pamoja na kumsisitiza awepo katika kikao hicho muhimu ameonekana kukaidi.

Katika idara ya maendeleo ya jamii kumebainika ukinzani wa taarifa baina ya zile zilizowekwa katika nyaraka za halmashauri na uhalisia kwa walengwa, ambapo inaonyesha vikundi vilivyopewa mikopo, hakuna hata kimoja kilichorejesha.


Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro wanasema mkanganyiko wa taarifa toka kwa watendaji na watumishi ni sula lililo zoeleka, wakisema miaka yote halmashauri inaendeshwa kwa matakwa ya upande mmoja.

Katibu tawala mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo anasema kinacho onekana ni watendaji kumdharau mkurugenzi wa halmashauri, ambapo hivi karibuni kuna baadhi ya watumishi walipewa barua za Mashtaka  na kuzichana mbele ya mkurugenzi muda mfupi baada ya kuzipokea.

Mbali na kuagiza kusimamishwa kazi kwa afisa mapato wa Halmashauri hiyo, mkuu wa mkoa huo Loata Ole Sanare ameagiza watendaji katika idara hizo mbili kupitia upya taarifa zote na kuzifanyia marekebisho kisha kuitisha kikao kingine, na kuja na taarifa za nani atagharamia kikao hicho.

Kikao hicho cha baraza maalum la madiwani ni mwendelezo wa utekelezaji wa agizo la waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi, kutaka wakuu wa miko kuwa wenyeviti wa baraza hilo kufuatilia kwa karibu taarifa za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali.



Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.